.

Thursday, August 12, 2010

SSSHHHH... KIJANA ACHA KULALAMIKA TUMIA KURA YAKO..!!


Telavisheni ya Afrika Mashariki (EATV) na East Afrika Radio kwa pamoja zimezinduwa kampeni ya kuhamasisha vijana kushiriki kikamilifua katika zoezi la upigaji kura katika uchaguzi mkuu wa oktoba mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana jijini Dar es salaam, kampeni hiyo ilizinduliwa katika kipindi cha 5 connect kilicho rushwa moja kwa moja kuanzia saa moja usiku na kuhudhuriwa na wageni vijana pamoja na mjumbe kutoka Tume ya Uchaguzi.

Kituo cha EATV ambacho ndio kituo namba moja kwa vijana na kimechukuwa jukumu hilo kuwahamasisha vijana kutumia kura yao, kutokana na utafiti uliofanywa na kituo hicho kuonyesha kuwa vijana wengi hawashiriki katika kupiga kura.

Katika kufanikisha hilo vituo vya EATV & EAR vitakuwa vinatumia ujumbe wa 'KIJANA ACHA KULALA MIKA TUMIA KURA YAKO' na ujumbe huo utakuwa ukirushwa hewani kupitia televisheni ya EATV na East Afrika Radio.

Ujumbe huu unalengo la kuhakikisha kijana anachaguwa kiongozi bora badala ya kuwaachia wengine shughuli ya kuchaguwa viongozi na badala yake kuishia kulalamika pindi wanapoona uamuzi mbali mbali wa viongozi unawaathiri.

Kampeni hii ambayo tumetumia picha za video na sauti za vijana mbalimbali itaendelea hadi Oktoba 30 na vile vile ifikapo septemba tutazinduwa kipindi maalum kwa ajili ya uchaguzi kiitwacho UCHAGUZI XPRESS LIVE.

Kipindi hicho tutajadili mada mbalimbali zenye lengo la kumjenga kijana ufahamu kuhusiana na umuhimu wa yeye kushiriki katika uchaguzi mkuu ili waweze kuchaguwa viongozi bora na wenye sifa.

2 comments:

  1. Hiyo itakuwa mzuka sana pia itahamasisha vijana wengi kupiga kura na kuchagua viongozi wanaowataka.EATV NA EARADIO MATING'A MAKALI NAMBA MOJA KWA VIJANA NAWAPENDA SANA.

    Naitwa joseph kyara.

    ReplyDelete
  2. tunakupenda pia mkaka... nawe pia unatakiwa kutumia kura yako na kuacha kulalamika...

    ReplyDelete

,