.

Tuesday, April 27, 2010

TULIFIKA MWANZA SALAAMA NA MAKAMUZI YAKAENDELEA.

Maneger masoko kutoka Zain Kelvin Twiser akiwasili katika jiji la Mwanza tayari kwa kuwapa wananchi uhuru wa kuongea kupitia Zain

Hawa ni wafanya kazi wa Zain ambao walikuja kutopokea Airport.

Huu sasa ni usiku wa J Martins ndani ya Villa Park na hawa ni mashabiki wa J Martins... palikuwa patam sana..

Huyu ni Dj Maliss wa Kiss FM alikuwepo naye kuto ushirikiano.

Wakazi wa Mwanza walifaudu vilivyo ndani ya Villa Park na J Martins.

Dj Ad a.k.a Mafuvu akisema na wana kutoka Mwanza.

Time ikafika na J Martins akakwea kwenye stage...



J Martins kwenye stage...

UHURU TOUR ILIANZIA DAR KWENDA MWANZA

Baada ya mchiz kukamua bongo pale makao makuu ya Zain ikafikia time ya kwenda Mwanza, Arusha kisha kurudi tena Bongo...

Dj Mafuvu, Domonicky Nyalifa na Dullah... hapo ni Airport tayari kabisa kukwea pipa mpaka Mwanza kwa ajili ya show ya J Martins.

Kelvin Twiser na J Martins story kidogo kabla ya kusepa kuelekea Mwanza.

Dj Kim akiwa kwenye mstari kabla ya kukaguliwa na kukwea.

Dullah na J Martins..

Dickson na Ngali.. hivi ni vichwa vingine kutoka EATV ingawa huwa hauvioni kwenye kideo.

Hawa ni jamaa wa Zain ambao nao pia walikuwa kwenye huo msafara wa kuelekea Mwanza

Dullah ndiye alikuwa mc wa show zote Mwanza, Arusha na Dar.

Time ya kuondoka ikafika tukawa tayari kuelekea kwenye ndege kwa ajili ya kuitafuta mwanza, ilikuwa safari ya kama saa moja na dakika hamsini na tano hivi.

Dj Kim ndani ya pipa..

A.Y na J Martins..

Mafu.. mafu.. mafuvu babyyyy....!!!

Chombo tayari kipo hewani kuitafuta Mwanza..

Thursday, April 22, 2010

HUU NDIO UHURU WA KUONGEA KUTOKA ZAIN

Leo kitanukishwa Mwanza ndani ya Villa Park, kesho itakuwa Arusha viwanja vya Triple A na kesho kutwa yaani juma pili itakuwa Dar-es-salaam bata zitaliwa pale Billicanas.. UHURU UNAO SASA.

Wednesday, April 21, 2010

HAYA NDIO MAANDALIZI KABLA YA MAKAMUZ YA J MARTINS

Nyalifa akiongea na moja kati ya wafanya kazi wa Zain.

Washkaji wakiweka mambo sawa ili wananchi waweze kuona live mchakato mzima jinsi utakavyoenda

Mipango ikiendelea.

Hawa jamaa ndio watakao sababisha live ya ITV pamoja na EATV.

Washkaji kutoka EATV Ombeni na Dominic Nyalifa ndani.

Yuleeeeee.....!!! mchiz anafanya ustaarabu wa maswala ya taa.

Hii ndio stage itakayo husishwa na burudani.

Tuesday, April 20, 2010

J MARTINS NDANI YA OFISI ZA ZAIN.

Hapa anatoa salaam kwa wafanya kazi wa ZAIN.

Hii ni picha ya pamoja J Martins pamoja na wafanyakazi wa Zain.




Hapa alikuwa ana sign autograph katika poster yake.

Thursday, April 15, 2010

HAWA NDIO BAADHI YA WASANII WALIO UWAGA UKAPERA.

Mmoja wa member anayeunda kundi la Wakali Kwanza, Joseph Mapunda a.k.a Qj pichani akiwa na mkewe Bi Elizabeth na kwa sasa wameungana na kuwa kitu kimoja kama Mr and Mrs Joseph Mapunda hii ni juzi tu jamaa kavuta jiko safi.

Huyu ni Matonya siku ya harusi yake hapo akiwa na rafiki yake kipenzi Banana Zoro pamoja na mkewe.. Na kwa kudra zake mwenyezi mungu ndoa hiyo imeshaipa baraka kwa kupatikana mtoto.. Tonya pia ni moja kati ya wasanii wa bongo flava ambao tayari washauwaga ukapera.


Picha juu ni Juma Nature na mkewe Pili siku ya harusi yao .. Sir Juma Nature na mkewe wamebarikiwa kupata mtoto wa kike aliyezaliwa katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke.. Huyu ni Mwingine pia ambaye amesha watoroka wale wengi ambao bado hawajakamilisha hili.


Baada ya vikao vingi vya kukamilisha hili na kupanga jinsi ya kulikamilisha hatimaye siku ikafika na kijana kutoka TMK Wanaume Family kuuwaga rasmi ukapera na kutuletea shemejiiiii.....!!! Ilikuwa siku ya jumamosi baada ya kuchukuwa kifaa jumla, hii ilikuwa katika kanisa la Azania Front jijini Dar es salaam.

Judith Wambura alizaliwa mkoani Shinyanga tarehe 15 jun, 1979 kwa Martha na Lameck Isambua Mbibo ambao ndio wazazi wake. Inasemekana dada jide alianza kuimba akiwa na umri wa miaka saba, alianza kuimba kanisani kama ilivyo kwa wasanii wengi, bi shosti pia ni moja ya wasanii wa bongo flava wanaoishi kwenye ndoa kwa sasa.

Banana Zorro na Suzy Walele wakilishana keki siku ya harusi yao iliyofanyika katika ukumbi wa Msasani Beach Club jijini Dar - es- salaam. Banana pia ni masanii wa bongo flava ambaye amesha sepa kwenye kundi la ukapera.

Na kwa sasa nadhani huyu ndio atakaye fata tunamuombea kila la kheri mungu ampe wepesi katika hilo Amin inshaallah.