.

Wednesday, March 31, 2010

BABA MZAZI WA QUICK RACKA HATUNAE TENA DUNIANI

Baba mzazi wa mwanamuziki wa hip hop bongo, Quick Racka amefariki dunia jana usiku majira ya sanne kasoro katika hospitali ya TMJ ambapo alikuwa amelazwa hapo.

Kwa maelezo ya Quick anasema mzee wake Charlse Mbanda alikuwa anasumbuliwa na presha ya kushuka na ilibidi kupelekwa katika hospitali ya TMJ kwa ajili ya matibabu zaidi na ndipo mauti yalipo mfika.


Msiba upo mbezi ambapo ndugu watakuwa hapo kwa ajili ya kuomboleza na mazishi ya mzee wetu mpendwa yatakuwa siku ya jomamosi.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONIO AMIN.

Tuesday, March 30, 2010

TID AJITOA KILI MUSIC AWARDS 2010

TID akiwa na mtoto wake.

Mchiz kutoka pande za kinondoni na pia ni kiongozi wa band ya Top Band Khalid Mohamed lakini sikio lako litakuwa limezoea jina la TID.

Amejitoa katika kushindania tunzo za Kili Music Awards katika upande wa Wimbo Bora wa Kiswahili kwa upande wa Band na sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kuwa mtu mzima anasema tunzo hizo hazimjengi.. Lakini kwa nyunyuziii.. zaidi kuhusu hili katiza pande za www.topbandtz.blogspot.com

Sunday, March 28, 2010

PLANET BONGO NA THE LAFAMILIA BAND.

Huyu mchiz ni mpiga dram kutoka the lafamilia band.. unamjuwaaaa...???

Wikii hii kipindi cha Planet Bongo cha EATV kilipata nafasi ya kutembelea kwenye moja ya show inayofanywa na band mpya na ya kwanza ya hip hop hapa bongo, band inayo ongozwa na Chidy Benz, ukitaka kujuwa nini kinafanyika usikose kuangalia PLANET BONGO kila juma tano saa tatu kamili usiku EATV Pekee.

Chid akiwa na wana kutoa EATV.

Huyu mchiz ni mpiga solo

The Lafamila Band mzigoni hapa ni Lamada Hotel.

Unamfahamu huyu...??? ni Dr. Kumpeneka yeye anaimba, anapiga dram na tumba pia kwa kifupi ni kifaa kingine kinachounda band hiyo.

Chid na Chiku Keto wakikamuwa.



Chek Planet Bbongo walivyo tega duuuh..

Thursday, March 25, 2010

HAWA NDIO WATAKAO WANIA TUNZO ZA KILI MWAKA HUU.

Hii ndio nembo ya Kili Music Awards kwa mwaka huu.

Mkurungenzi masoko wa TBL Bw. David Minja akiwa na meneja wa Kilimanjaro bia Bw. Georger Kavishe wakiwa katika mkutano wa kutangaza wasanii walio ingia katika vinyang'anyiro vya tunzo za Kili mwaka huu.

Wanaowania tunzo ya Mwimbaji bora wa kike.

Lady Jaydee
Mwasiti Almasi
Maunda Zorro
Vumilia Mwaipopo
Khadija yusuphu

Wanaowania tunzo ya Mwimbaji bora wa kiume

Marlow
Banana Zorro
Mzee Yusuphu
Ally Kiba
Christian Bella

Wanaowania Albamu Bora ya Taarab

Jahazi Modern Taarab (Daktari wa Mapenzi),
Five stars Modern Taarab (Riziki mwanzo wa chuki),
Coast Modern Taarab (Kukupenda isiwe tabu),
New Zanzibar star (Powa mpenzi),
East African Melody (Kila mtu kivyakevyake).

Tunzo ya Wimbo Bora wa Taarab inawaniwa na

Daktari wa mapenzi (Jahazi Modern Taarab),
Roho mbaya haijengi (Jahazi Modern Taarab),
Msitujadili na Riziki mwanzo wa chuki (zote Five stars Modern Taarab),
Kupenda isiwe tabu (Coast Modern Taarab).

Tunzo ya Wimbo Bora wa Mwaka inawaniwa na

Marlow (pii pii - Missing my baby),
Diamond (Kamwambie),
Banana Zorro (zoba),
Hussein Machozi (Kwa ajili yako).

Tunzo ya Wimbo Bora wa Kiswahili kwa upande wa bendi ni

Machozi Band (Nilizama),
African Stars Band - 'Twanga pepeta' (Mwana Dar es salaam),
Top Band (Asha),
FM Academia (Vuta nikuvute),
Extra Bongo (Mjini Mipango).

Tunzo ya Albamu Bora ya Bendi inawaniwa na

African Stars Band - 'Twanga pepeta' (Mwana Dar es salaam),
Kalunde Band (Hilda),
Msondo Ngoma Music Band (Huna Shukrani).

Tunzo Bora ya Wimbo Bora wa R&B wanaowania ni

Belle 9 (Masogange),
Diamond (Kamwambie),
A.T na Stara Thomas (Nipigie),
Maunda Zorro (Mapenzi ya Wawili),
Steve (Sogea Karibu).

Tunzo ya Wimbo Bora wa Asili ya Kitanzania inawaniwa na

Mrisho Mpoto (Nikipata Nauli),
Machozi Band (Mtarimbo),
Offside Trick (Samaki),
Wahapahapa Band (Chei Chei),
Omari Omari (Kupata Majaaliwa).

Wanaowania Tunzo Wimbo Bora wa Hip Hop ni

Joh Makini (Stimu Zimelipiwa),
Quick Racka (Bullet),
Chid Benz (Pom pom pisha),
Mangwea (CNN),
Fid Q (Iam a professional).

Tunzo ya Wimbo Bora wa Reggae inawaniwa na

Hemed (Alcohol),
Dabo Ft. Mwasiti (Don't Let Go),
Man Snepa (Barua),
Matonya Ft. Christian Bella (Umoja ni Nguvu).

Kwa upande wa Wimbo Bora wa Ragga, wanaowania ni

Dully Sykes (Shikide),
Bwana Misosi (Mungu yupo bize),
Drezzy Chief (Wasanii),
Benjamin wa mambo jambo (Fly).

Tunzo ya Rappa Bora wa Mwaka inawaniwa na

Chokoraa
Ferguson
Kitokololo
Totoo ze bingwa
Diouf

Tunzo ya Msanii Bora wa Hip Hop ni

Joh Makini
Chid Benz
Mangwea
Profesa jay

Tunzo ya Wimbo Bora wa Africa Mashariki inawaniwa na

Blue 3 Ft. Radio and Weasal (Where you are),
Kidum Ft. Juliana (Hturudi nyuma),
Cindy (Na Wewe),
Radio and Weasal (Bread and Butter),
Kidum (Umenikosea).

Tunzo ya Mtunzi Bora wa nyimbo ni

Mzee Yusuphu
Mrisho Mpoto
Lady Jyadee
Banana Zorro

Tunzo ya Mtayarishaji Bora wa Muziki ni

Lamar
Marco Chali
Hermy B
Allan Mapigo
Man Water

Video Bora ya Muziki wa Mwaka inawaniwa na

Lady Jaydee (Natamani kuwa Malaika),
Diamond (Kamwambie),
AY (Leo),
Banana Zorro (Zoba),
C Pwaa (Problem).

Tunzo ya Wimbo Bora wa Fro Pop inawaniwa na

Banana Zorro (Zoba),
Ally Kiba (Msiniseme),
Marlow (Pii pii - Missing my baby),
Mataluma (Mama Mubaya),
Chegge (Karibu kiumeni).

Tunzo ya Msanii Anayechipukia
Belle 9
Diamond
Barnaba
Quick Racka
Amini

Tunzo ya Wimbo Bora wa Kushirikiana unawaniwa na

AT na Stara Thomas (Nipigie),
Mangwea na Fid Q (CNN),
Barnaba na Pipi (Njia Panda),
Mwana FA na Profesa Jay na Sugu (Nazeeka Sasa),
Hussein Machozi na Joh Makini (Utaipenda).

Monday, March 22, 2010

HUYU NDIO SAM WA POWER JAMS YA EAST AFRICA RADIO.

Msikilize kila juma tatu mpaka ijumaa kuanzia saa saba mchana mpaka saa kumi alasiri.

MAKAMUZI YA KIDUM BONGO.

Hawa ndio walio sanukia mchongo huo na walifurahia mzigo ulio pigwa na Kidum.

Tofauti na Kidum pia kulikuwa na burudani kutoka kwa vijana wanao cheza.

Tawakal mzigoni.



duh... mashine begani... huyu jamaa anaitwa Tawakal ni mpiga picha wa EATV.

Kidum alikuwa na jumu moja tu.. la kuhakikisha raia wanafurahi na kwakweli alifanikiwa katika hilo.

Kidum akiwa kwenye stage na msanii wa muziki wa kizazi kipya Marlaw, pia Kidum amedhihirisha kuwa huyo ndio msanii anayemkubali.




Mchiz kamaa.. Carlos Santana jinsi alivyo miliki hilo gitaa.. ni moja kati ya wanao unda band ya kidum.

Dominic Nyalifa yupo na shabiki wake katika show ya Kidum Sun Cirro club.

Baada ya Kidum kumaliza zilidondoshwa kopo kutoka kwa ma dj wa East Africa Radio.

Hii ndio band ambayo Kidum anafanya nayo kazi.

Huyu ni shabiki wa kipindi cha Afro Beat ambacho ndio kilidhamini onyesho hilo la Kidum..

Sunday, March 21, 2010

MCHAKATO WA KILIMANJARO MUSIC AWARDS 2010.

Hii ndio nembo ya Kili Music Awards kwa mwaka 2010

DJ Choka, Millard Ayo na Dullah wakiwa nje ya ukumbi

Wadau mbalimbali wakibadilishana mawazo.

Wakati wa msosi ulifika wadau walihusiki kikamilifu.

Friday, March 19, 2010

KABLA YA KUKAMUA LEO USIKU ALIKUJA MZIGONI KWANZA.

Leo ndio siku ambayo mtu mzima KIDUM atakinukisha pande za sinza katika club ya Sunn Cirro. Usiku wa leo utakamilika pale kwa kukutana na watu tofauti kutoka sehemu mbali mbali katika jiji hili la Bongo kingilio ni 15,000 kwa upande wa chini wa kawaida na 20,000 kwa upande wa pili wa V.I.P.
Leo asubuhi alikuja mzigoni kwa ajili ya kuongea na raia wa Africa Mashariki kuhusu show ya leo.

Hapa alikuwa anaongea na wana africa mashariki kupitia EATV leo asubuhi.

Hilo linaitwa gwala linawahusu wale wote amabo tutakutana paleeee... pande za sinza sunn cirro club.

Na ukafika wakati wa kuongea na wana africa mashariki kupitia East frica radio leo asubuhi.

SUGU ABURUZWA KWA PILATO..!!

Kesi hiyo iliyofunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dsm, ni kutokana na kauli ya msanii huyo kwamba kampeni iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam, Februari 13 mwaka huu dhidi ya malaria, ilitokana na wazo lake.

Kesi hiyo iliyoko mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Joyce Minde, MNM wanawakilishwa mahakamani hapo na Kampuni ya Uwakili ya Excellent Attorney and Advocates ya jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka ya kesi hiyo, mlalamikaji ameieleza mahakama kuwa msanii huyo na washirika wake, Deiwaka Entertainment na William Mungai, hawana mamlaka na haki zozote za kisheria kwenye mradi huo.

Aidha, kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi ya msingi, walalamikaji wamewasilisha ombi la awali la kutaka mahakama kumzuia Sugu kuitisha mkutano wowote na vyombo vya habari kuhusiana na suala hilo. Kesi hiyo itaanza kusikilizwa Machi 24, mwaka huu.

Hivi karibuni, Sugu alidai kuwa waandaaji wa kampeni hiyo ya ‘ZINDUKA Malaria Haikubaliki,’ iliyozinduliwa katika viwanja vya Leaders, Dar es Salaam na Rais Jakaya Kikwete, hawakumshirikisha, hivyo kuiba wazo lake.

Mradi huo unaolenga kutoa ujumbe wa kupambana na malaria, umekuwa na utata kuhusu nani alibuni wazo hilo, kwani Sugu anadai ni wazo lake la muda mrefu.

Taasisi ya MNM ni asasi ambayo imekuwa ikifanya kazi zake tangu mwaka 2006 ya kukomesha malaria barani Afrika na imekuwa ikishirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii tangu mwaka juzi ikisambaza vyandarua 267 katika kampeni ya taifa ya kukinga watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.

Kwa mujibu wa MNM, kampeni hiyo ilisifiwa kwa mafanikio ikiwa na lengo la kupeleka ujumbe kwa Watanzania kwamba malaria inaweza kukingwa na kutibiwa.

Sugu katika madai yake, alisema alitoa wazo la kushirikisha wasanii katika kampeni hiyo lakini wakati maandalizi yanafanywa hakuhusishwa hadi kupatikana kwa wasanii zaidi ya 20 walioshiriki.

MNM katika taarifa yake, ilisema mwaka juzi Mkurugenzi wake wa Mawasiliano, Martin Edlund, alikutana na Sugu kwa bahati ndani ya ndege wakiwa safarini kuja Tanzania.

“Martin alikuwa katika ziara ya utafiti wa kupata watu wazuri ambao wangeweza kusaidia katika kuandaa kampeni ya kitaifa dhidi ya malaria ... hatua kama hiyo ilishafanyika nchini Senegal kwa kushirikiana na mwanamuziki nguli, Youssou N’Dour,” ilisema taarifa.

Ilisema MNM awali ilitambulishwa kwa Kampuni ya matamasha nchini ya Round Trip, na mshirika wa kibiashara wa Sugu aitwaye William Mungai wa Kampuni ya Deiwaka Entertainment.

“Baada ya utafiti wa kina, Round Trip ilitambuliwa kama kampuni inayoweza kuitangaza na hata kuandaa uzinduzi wa kampeni hiyo na kusaini mkataba na MNM mwaka jana. “Si Sugu wala Mungai waliohusishwa katika mpango wa uzinduzi wa tamasha la ZINDUKA,” ilisema taarifa.

Iliongeza kuwa MNM pia ilifanya utafiti wa kupata wasanii waliopo nchini na kuamua kuwa itashirikiana na wasanii Profesa Jay, Bi Kidude, Lady Jaydee, Banana Zorro, THT, Mwasiti na Marlaw, ili kusambaza ujumbe wa kupambana na malaria nchini kama sehemu ya mkakati wa kufanikisha kampeni hiyo.

Ilisema MNM si asasi ya kutengeneza faida na imekuwa ikifanya kazi yake tangu mwaka 2006 ya kukomesha malaria barani Afrika na imekuwa ikishirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii tangu mwaka juzi, ikisambaza vyandarua 267 katika kampeni ya taifa ya kukinga watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.

Monday, March 15, 2010

HIKI NI KICHWA KIPYA KATIKA MUZIKI WA HIP HOP.

Ni Herieth binti mdogo sana katika muziki huu wa hip hop hapa bongo. Ambaye anaamini anauwezo mkubwa sana wa kuchana lakini bado hajapatiwa nafasi ya kuonyesha uwezo wake na ndio mana MPANGO MZIMA imempa hili shavu la kuwepo hapa leo.

Ngoma yake ya kwanza alifanya na Linex inaitwa
wanapo sikia ni moja kati ya ngoma ambazo ameonyesha uwezo mzuri sana, lakini kwa sasa yupo katika harakati za kushusha mkwaju mwingine mpya unaitwa "PUT YA GUNZ DOWN". Sikiliza Planet Bongo jumamosi kuanzia saa nne asubuhi East Africa Radio.

Sunday, March 14, 2010

RM Barber Shop

Ni Saloon ya kisasa yenye vyombo vya kisasa na huduma bora kwa wateja wake.
-Scrub
-Magic
-Super Black
-Wave
-Mask
-Facial
-Manicure
-Pedicure
-Steam
Ipo Barabara ya long bagamoyo road Mbezi Beach ukifika daraja la kawe kwenye Round about inayokata kushoto basi kuelekea kawe unaiyacha unanyoosha moja kwa moja zamani ilikuwa barabara ya vumbi kwa sasa ina lami

Saturday, March 13, 2010

BAADA YA KUTOKA MUHIMBILI SAFARI ILIKUWA STUDIO KWA MANEKE.

Ilifika zam ya k-sher kutoa hisia zake kwenye mic.

Dhumuni kubwa la kwenda kwa maneke ni kutengeza wimbo kwa ajili ya huu msiba na wimbo huo alifanya K - Sher, Hussein Mchozi pamoja, Tunda Man na mimi mwenyewe dazin kamaa nilihusika hivii.


Huyu ni Maneke producer ambaye ndiye aliyefanya hiyo kazi.

K-Sher na Maneke wakati wa kutengeneza wimbo huo.

Producer Maneke akitoa maelekezo jinsi ya kufanya

Tunda Man na Hussein Machozi wakiwa kwenye mazoezi mafupi kabla ya kuingiza sauti.

Thursday, March 11, 2010

POLE SANA NDUGU YANGU MADEE..

Madee akiwa na Pendo
Dah... Madee kwa sasa yupo kwenye wakati mgumu sana baada ya mpenzi wake kipenzi Pendo kufariki katika ajali ya gari iliyo tokea jana dodoma.

Pendo alikuwa anatoka dar kwenda dom kwa ajili ya kuendelea na masomo lakini kwa mipango ya mungu ndio haya yametokea, kwa sasa mwili wa marehemu upo hospitali ya Tumbi, nitakufahamisha zaidi baadaye kidogo
.

Picha hii nimeitoa kwa anko michuzi ni taswira ya hiyo ajali.