PLANET BONGO KILA JUMAMOSI SAA NNE ASUBUHI EAST AFRIKA RADIO NA KILA JUMA TANO SAA TATU KAMILI USIKU EATV.
KUWA MAKINI
TULIA NA MMOJA UNAYE MPENDA, ACHA NGONO ZEMBE
POWER JAMS
POWER JAMS,JUMATATU MPAKA IJUMAA KUANZIA SAA 7 MCHANA HADI 10 ALASIRI EAST AFRICA RADIO.
MATING'A
DEEJAY AD a.k.a MAFUVU.
KUTANA NA DEEJAY AD KWENYE POWER JAM KILA J.3 NA ALHAMISI (1:00 - 4:00 pm), THE CRUISE J5 (8:00-9:00 pm), PLANET BONGO JUMAMOSI (10:00 - 12:00 pm) & FNL. NDANI YA EAST AFRICA RADIO & TV, TING'A KALI NAMBA MOJA KWA VIJANA
SIKILIZA EAST AFRICA RADIO KILA JUMAPILI SAA 10 - 12 JIONI KWA NGOMA KALI ZA LONG TIME KAMA SHOULD I SAY YES,NIGHT SHIFT,LET'S GO DANCING,ELLUSION NK NA DJ 45 KING...WAY BACK HITS!
Lile ting'a kali no 1 si ndo' limerudi tena babu....kila siku za Jumatatu na Alhamisi mida ya saa 3 usiku usikose kukodolea mimacho runinga yako Live!!!!
Rais wa Manzese,Madee ataliongoza baraza lake la wasanii siku ya Idd pande za Club San-Siro maeneo ya Sinza kwenye uzinduzi wa album mpya ya kundi BADO TUNAPANDA.
Wana watasindikizwa na vichwa vikali kama Godzilla,Jahfaray,Mwasiti,Lina,Young D na Roma.
Ni jamaa ambaye amelalamika sana kuhusu mama watoto wake anafahamika kwa jina la Mama Halima kuwa amemtenda sana na hakutegemea hilo kwa bi shosti huyo.
Mchiz anaitwa Linex ambaye ngoma yake ya Mama Halima inafanya vzr sana kwa sasa kwenye Radio station nyingi za hapa bongo.
Sasa mpango mzima ni kuwa kideo cha ngoma hiyo kinachapwa leo na mtu mzima JOHN KALLAGE na siku si nyingi kitaanza kuwa hewani kupitia EATV..
Telavisheni ya Afrika Mashariki (EATV) na East Afrika Radio kwa pamoja zimezinduwa kampeni ya kuhamasisha vijana kushiriki kikamilifua katika zoezi la upigaji kura katika uchaguzi mkuu wa oktoba mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana jijini Dar es salaam, kampeni hiyo ilizinduliwa katika kipindi cha 5 connect kilicho rushwa moja kwa moja kuanzia saa moja usiku na kuhudhuriwa na wageni vijana pamoja na mjumbe kutoka Tume ya Uchaguzi.
Kituo cha EATV ambacho ndio kituo namba moja kwa vijana na kimechukuwa jukumu hilo kuwahamasisha vijana kutumia kura yao, kutokana na utafiti uliofanywa na kituo hicho kuonyesha kuwa vijana wengi hawashiriki katika kupiga kura.
Katika kufanikisha hilo vituo vya EATV & EAR vitakuwa vinatumia ujumbe wa 'KIJANA ACHA KULALA MIKA TUMIA KURA YAKO' na ujumbe huo utakuwa ukirushwa hewani kupitia televisheni ya EATV na East Afrika Radio.
Ujumbe huu unalengo la kuhakikisha kijana anachaguwa kiongozi bora badala ya kuwaachia wengine shughuli ya kuchaguwa viongozi na badala yake kuishia kulalamika pindi wanapoona uamuzi mbali mbali wa viongozi unawaathiri.
Kampeni hii ambayo tumetumia picha za video na sauti za vijana mbalimbali itaendelea hadi Oktoba 30 na vile vile ifikapo septemba tutazinduwa kipindi maalum kwa ajili ya uchaguzi kiitwacho UCHAGUZI XPRESS LIVE.
Kipindi hicho tutajadili mada mbalimbali zenye lengo la kumjenga kijana ufahamu kuhusiana na umuhimu wa yeye kushiriki katika uchaguzi mkuu ili waweze kuchaguwa viongozi bora na wenye sifa.
RIP NELSON CHRIZOSTOM BUCHARD AKA FAZA NELLY (1976-2006)
Kundi la Watengwa toka A-Town chini ya JCB wametoa audio na video ya kumkumbuka mwanaharakati na memba wa X-Plastaz,Faza Nelly ambaye alifariki 29 March 2006 kwa kuchomwa kisu Mkoani Arusha iitwayo "SITOWASAHAU MILELE"
Ndani ya ngoma hiyo pia wamekumbukwa wanaharakati kibao wa muziki wa Tanzania (REST IN PEACE..BROS & SISTAZ)
NI WEWE KAMPENI, MAENEO YA ITUNUNDU PAWAGA JANA
-
Ni Wewe ni kampeni iliyozinduliwa na redio Ebony FM iliyoko Nyanda za juu
kusini, ikiwalenga zaidi wananchi wa vijijini ambao miundo mbinu ya umeme ...
HARD PRICE COMING SOON
-
* Samahanini sana wadau wangu... Naombeni sana mnisamehe kwa kupotea kwa
kipindi kirefu, na yote haya yanatokana na majukumu ya hapa na pale. Ila
nisinge...