Baba mzazi wa mwanamuziki wa hip hop bongo, Quick Racka amefariki dunia jana usiku majira ya sanne kasoro katika hospitali ya TMJ ambapo alikuwa amelazwa hapo.
Kwa maelezo ya Quick anasema mzee wake Charlse Mbanda alikuwa anasumbuliwa na presha ya kushuka na ilibidi kupelekwa katika hospitali ya TMJ kwa ajili ya matibabu zaidi na ndipo mauti yalipo mfika.
Msiba upo mbezi ambapo ndugu watakuwa hapo kwa ajili ya kuomboleza na mazishi ya mzee wetu mpendwa yatakuwa siku ya jomamosi. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONIO AMIN.
SOMALIA YAAMUA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KATIKA UNUNUZI WA BIDHAA ZA AFYA
-
Rais wa Somalia Mheshimiwa Hassan Sheikh Mohamud amesema nchi yake imeamua
kushirikiana kwa karibu na Bohari ya Dawa ya Tanzania katika ununuzi wa
bidhaa...
11 minutes ago