.

Monday, February 15, 2010

BEEZY MCHIZ AMBAYE AMEGAWA SHAVU KWA WANA.

Mix Tape ipo tayari na mchiz ameamuwa kugawa shavu kwa wana, ametowa nafasi ya ku- download Mix Tape yake ya THE B-DAY. Kama wewe ni mpenz wa muziki una nafasi hiyo cha kufanya ni kuingia www.beezy-music.com kwa ajili ya kusikiliza Mix Tape hiyo pamoja na ku- download.

Beezy akiwa Abby katika moja ya show zake hap bongo.

Huyu ndio Beezy mchiz ambaye yupo nje ya bongo lakini anaendeleza harakati za bongo flava.

Sunday, February 14, 2010

HUU NDIO MZIGO MPYA WA FID Q..


Hii ni albam mpya ya Fid Q kaa tayari...!!!!

Saturday, February 13, 2010

MAMA MZAZI WA G- SOLLO AFARIKI DUNIA.

Mama yake mzazi msanii wa hip hop bongo G-Sollo amefariki dunia saa 5, usiku wa kuamkia leo mkoani Iringa, Shughuli zote za mazishi zinafanyika Dodoma nyumbani kwao G-Sollo.

G-Sollo leo ilikuwa azinduwe kitabu chake cha 'HARAKATI ZA BONGO FLAVA NA MAPINDUZI' kwenye tamasha la Sauti za Busara lifanyikalo Zanzibar.
Mpango mzima inampa pole G-Sollo na ipo naye pamoja katika kipindi hiki kigumu cha maombelezo.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMIN.

Friday, February 12, 2010

UMESHAJUWA PAKWENDA MKESHA WA VALENTINE DAY....???? NI MZALENDO PUB HAKUNA KWINGINE.

Huu ni wakati wa kumonyesha mapenzi ya dhati yule unaye mpenda kwa kumfanyia mambo mengi mazuri moja wapo likiwa ni kumpeleka sehemu nzuri, tulivu na yenye burudani. Ushapafahamu ni wapi..??? ni MZALEND PUB ni jumamosi tarehe 13 usiku wa kuamkia Valentine day.

MISHE ZA ZE COMEDY SEARCH...

Hawa ni baadhi ya vijana waliojitokeza, hapa wapo ndani kwa ajili ya kujiandaa kuonyesha uwezo wa katika kuchekesha.

Kwenye stage mchiz anawajibika... jukumu ni moja tu kuhakikisha kila kichwa kilichomo humo ndani kina cheka... duh... ilikuwa kazi...!!!

Humu ndani ndio vijana walionyesha uwezo wao.

Wana kutoka sehemu mbali mbali walikuja kujaribu bahati zao.

Kulikuwa na kazi ya kutowa maelezo, mtu unamwambia kitu cha ukweli yeye analeta comed dah... shughuli ilikuwa ngumu sana.

Hapa wanaelekea kwenye kujisajili kisha kusubiri kuingia ndani kuonyesha uwezo wao.





Hapa sasa ndio wanajisajili kabla ya kuingia ndani.

Moja kati ya washiriki akitowa maelezo wakati wa kujisajili.

Mchiz inabidi asome fom kwa umakini na baada ya kuelewa ndio ajaze.



Huyu mama anaitwa Asha Boko wengi mnamfahamu naye alikuwepo katika mchakato huu.

Hawa ni Sunche na Kapeto nao ndani.

Haya sasa.... si unamuona hapo Bambo na Kingwendu wakiwa katika foleni ya kwenda kuji sajili.

Huyu jamaa me alinifurahisha na hizo nywele zake duh..... kulikuwa na vituko sana.

Mpango mzima ulikuwa New World Cinema, ambapo vijana wengi sana walijitokeza kwa ajili ya kuonyesha uwezo wao katika fani ya uchekeshaji, EATV inarudisha tena kipindi cha Ze Comedy na huu ndio mchakato wa kutafuta watu ambao watafanya kipindi hiko.

Wednesday, February 10, 2010

BEBE COOL ANAKOMAA NA FIDIA..

Mwanamuziki Moses Ssali a.k.a Bebe cool amefunguwa kesi ya madai kiasi cha shillingi millioni mia nane ya Uganda kama fidia. Bebe Cool pamoja na walinzi wake walipigwa risasi hivi karibuni baada ya kuzuka vurugu baina yao na polisi.

Msanii huyo amedai kuwa serikali ndio inawajibika kwa vitendo vya polisi hao. Madai hayo yameandikwa kuwa msanii huyo anategemea maonyesho yake kupata kipato chake na kwa kuwa inawezekana akakaa kitandani kwa muda wa miezi sita na zaidi anataka alipwe kiasi hicho cha fedha kama fidia.

JORDIN SPARK ABUNI CHENI KWA AJILI YA HAITI.

Msanii Jordin Sparks akisaidiana na mbunifu wa vito Tim Foster, amebuni cheni yake ambapo fedha zitakazo patikana baada ya mauzo ya cheni hiyo zitasaidia wahanga wa Haiti.

Cheni hiyo inatarajiwa kuuzwa kwa dola 125 na asilimia 30 ya mapato itaenda katika mfuko wa msaada wa msanii huyo.
Jordin pia ni moja kati ya wasanii walioshiriki katika kurekodi kwa mara ya pili wimbo wa 'We are the World' .

NGOMA YA WYRE NA COOZOS CLAN ON AIR.

Wimbo ambao msanii nyota wa Kenya Wyre ameshirikiana na kundi la Coozos Clan kutoka Sudan umeshatoka. Wimbo huo ambao ulirekodiwa mwishoni mwa mwaka jana kwa sasa unafanya vizuri sana nchini Kenya, na kundi hilo kwa sasa lipo nchini humo kwa ajili ya kujitangaza.

Monday, February 8, 2010

JAMBO NI MOJA TU LAKUFANYA... HILI HAPA..

Hii itakuwa Alhamis kuanzia saa 3 asubuhi hapa ndipo watapatikana watakao chukuwa jukumu kutuvunja mbavu katika kipindi cha Ze Comedy. Je... wewe ni mmoja wao....?????