.

Tuesday, April 13, 2010

BAADA YA UKIMYA WA TMK WANAUME HALISI

Kundi la TMK HALISI limesaini mkataba na kampuni inayoitwa DLC ambayo inafanya biashara zake China na Tanzania, kampuni hii ambayo yenyewe ndiyo itasimamia kila kitu ikiwemo mambo ya promosheni kutafuta maonyesho ya nje na ndani ya nchi pia kusimamia mauzo ya kila kitu.

Kiongozi wa kundi hilo Juma Kassim Nature,andai kuwapata wakati mgumu sana kuchuja na kuchagua vichwa vinne atakavyo fanya navyo kazi ya kuunda TMK Halisi mpya yenye vichwa vitani akiwemo yeye...badala ya ile ya awali iliyokuwa na wasanii 12.


Walio chaguliwa kusaini mkataba huo ni DOLO, BABA LEVO,JB WA MABAGA FRESH,KG SON pamoja na Juma Nature mwenyewe.


Mpaka tunakwenda mitamboni kundi hilo linalodhamiria kurudi upya baada ya kufulia kwa muda wa kutosha katika anga ya muziki wa kizazi kipya,limeshafanya kazi inayoitwa MNATAKAJE? ambayo imeanza kusambazwa redioni tangu mwishoni mwa wiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment

,