Mchizi kutokea Morogoro Afande sele ameamuwa kuweka wazi hisia zake kuhusu mchiz kutoka Arusha Joh Makini pamoja na Rais wa Manzese Madee. Afande Sele ametowa hisia zake hizo wakati alipokuwa anauzungumzia wimbo wake mpya wa KINGDOM wimbo ambao amezungumzia mambo mbali mbali yanayo husu muziki huu. Afande aliuzungumzia wimbo wa Joh Makin wa "NIAJE NIVIP" kuwa ni wimbo ambao mchiz ametumia maneno ya kudhalilisha, wanawake wa nchi masikini kama Tanzania ambao ni mashabiki wa hip hop na Bongo flav.
Alitolea mfano katika ubeti wa Nik wa Pili katika huo wimbo kuwa "washindi wa tuzo za kili wanavuja kama fistula, jipime kama una tundu nyuma ya kaptula" anasema "huwo ni ubeti unao wazalilisha wanawake, hawa wagonjwa wa fistula hawakupenda kuwa hivyo" alisema Afande.
Kwa upande wa Madee alipaka mbayaa.. kuhusu Madee na kusema kuwa "huwezi kujiita Rais wa manzese wakati unaimba matusi, Rais gani unatukana hovyo, Rais gani huna ofisi..?? Wewe unajiita Rais lakini unaimba vitu vya kipuuzi ambavyo mtu akisikia anaona kabisa kuwa ulikurupuka" hayo ni maneno ya Afande Sele kwa Madee.
Mwisho Afande Sele alitoa ushauri kwa wasanii wote kuwa wasiige mambo ya ki- Marekani ambayo hayawasaidii, na si kila kitu anacho fanya msanii wa Marekani sisi tukifanye tubadilike"
WAZIRI MKUU AKAGUA SHAMBA LA MKULIMA WA KAKAO, KYELA
-
Waziri Mkuu Kasssim Majaliwa leo Mei 12, 2024 ametembelea shamba la Mkulima
zao la Kakao Clement Msalangi lililopo kijiji cha Mababu, Wilayani Kyela
Mei 12...
42 minutes ago
No comments:
Post a Comment
,