.

Tuesday, July 27, 2010

Saturday, July 24, 2010

MWANA ADAI KAIBIWA BEAT YA "USIJE MJINI"

Mchizi anajulikana kama Nazir Ally AKA Naz D (shati jekundu) toka pande za Zenji ameibuka na kudai kuwa Beat ya Usije Mjini ambayo wana AY & FA wametia mavocco humo ndani ni mali yake na aliinyonga Producer Pancho na Pancho ameitoa bila ridhaa yake,na yeye kudai kua haina kwere ila yeye nae atatoa ngoma kwa beat hiyo hiyo.....na atakuja mjini na track yake!!!

Wednesday, July 14, 2010

AL BATA...MARUFUKU KULIWA ZENJI!

Wimbo wa Mhhhh Mhhhh....Al Baaaataaaa toka kwa Offside Trick umepigwa marufuku visiwani Zanzibar.

Kwa mujibu wa mmoja wa memba wa kundi hilo,Lil Ghetto wimbo wa Al Bata umepigwa marufuku kupigwa kwenye Radio Stations zote,Night Club,pamoja na Video yake pia kutokuoneshwa na tangazo hilo pia limetolewa kwenye runinga ya TVZ.....Nyunyuz zinadai kuwa hata wimbo wa "AHMADA" nao umefungiwa kwa kua eti unamlenga mmoja wa kiongozi wa ngazi za juu visiwani humo....NISIJE NIKAKOSA MIEEEEE.....NIKAKOSAAAAA!

TEENS...YOUTH....DONT MISS THIS..!!!

We need new leaders of industries and God is putting you up in that position...don't Miss out this!......Teens.....Youth.....are gonna be in the House.....come and hear Words that will change your Destiny... ....new politician are been raised and you are among them ,new Doctors ,Business men and women....The future is yours....Your a Doctor with a difference...a lawyer with a difference...a manager with a difference.....an accountant with a difference a banker with a difference...I know who i am........The future is mine......Glory to God...!!!!!!!

don't Miss this Special online Conference with Pastor Chris..Teens and Youth around the World will be connected on that Day be a apart of this great movement.

Bring a long with you, Your brothers and sisters..your cousins, your Children...your friends Children, your big sisters and big brothers, your friends...your friends friends...Ur Future will never remain the same

Come and experience The Word The praise and Worship,The Dancing and Drama...Free Drinks and Snacks will be available also ..............

BREAKING NEWS...ABUU FLAVA NINI TENA!!


Msanii Chipukizi wa Bongo Flava,Abuu Flava ameshitakiwa COSOTA na Mwanamuziki Diamond kwa kosa la kutoa wimbo wake wa Kafara ukiwa unafanana melody na ule wa Diamond,Mbagara.

Na jana ndio ilikua ni siku ya kutolewa hukumu japo Diamond hakufika hata siku moja kwenye kikao cha usuluhishi...na haya yalifikiwa...

1. COSOTA watatoa matangazo kwa FM Radio zote kupiga marufuku wimbo wa KAFARA usichezwe tena!

2.Itabidi Abuu Flavaa amlipe fidia msanii Diamond kama akitaka.

POLE MWANA BUT KAMA KUNA PRODUCER YOYOTE YUKO TAYARI KUMSAIDIA DOGO KIMUZIKI AWASILIANE NAE KWA No: 0652131651 KWANI ANA TALENT NA ANAWEZA KUFANYA VIZURI KWENYE GAME!!!!!!!!

Tuesday, July 13, 2010

MMHH...MWENZANGU!

....Hata Tabolaaa hamna hiii!!!!

DUH...MWANA ALITAKA KUSEPA NA WORLD CUP??




PWEZA ATUNUKIWA KOMBE LA DUNIA

Pweza aliyejipatia umaarufu duniani kwa kutabiri "mia" mechi za kombe la dunia 2010,Paul ametunukiwa kombe la dunia na mmiliki wake anasema kwa sasa amestaafu utabiri na anakula bata tu....kwenda mbeeeeleeee!

CHAMELEONE NA SHAKIRA DAM DAM!

Mwana toka Uganda,Jose Chameleone akiwa na Shakira kwenye maandalizi ya show ya fainali la kombe la Dunia 2010 na alipiga show ya kutakata...hakwenda na maji!

NAMELESS AZUSHIWA KIFO!

Habari zilisambaa jana kwenye mtandao wa Facebook kuwa Nameless amepata ajali mbaya ya gari Mombasa lakini habari za kuaminika zinasema mwana mzima wa afya na yuko Malindi akijiandaa kupiga show kadhaa...POLE JO!!!

Monday, July 12, 2010

WAHU NAE ALA BATA KWA OBAMA



Shemeji yetu kwa Nameless,Mwanamuziki Wahu toka Kenya yuko kwenye tour nchini Marekani.
Si unakumbuka mipini ya Sweet Love na Running Low?...hapo juu wana wakilishwa bata mjini Kansas na atakua huko kwa wiki tatu..!

BATA ZA AY & FA...NDANI YA ULAYA!!!

SPAIN BINGWA WA DUNIA 2010

Nahodha wa Spain,Iker Casillas akinyanyua Kombe la Dunia baada ya kuibonda Timu ya Holland 1 - 0

Thursday, July 8, 2010

CHAMELEONE NA BEENIE MAN WATOA NGOMA!

Jose Chameleone toka Uganda na King Of DanceHall,Beenie Man "mjukuu wa Baba T" toka Jamaica wametoa ngoma kali iitwayo..."How We Go" wakiwa wamempa shavu Jacky toka Blu 3.

Chameleone na Jacky walitupia ma-vocco Dreams Studio-nchini Uganda na kuyapeleka Jamaica na Beenie Man kumalizia mpango mzina na mzigo kwa sasa inapata shavu la kutosha kwenye redio nchini Uganda......................na kupitia EA Radio utaisikia kwa mara ya first!!!

..WE USIJE MJINI...WAO WANAENDA ULAYA!!!

...Hivi ni kweli wewe USIJE MJINI halafu wao wanakwenda kupiga Tour Europe???!!

"Mapacha Wasiofanana" Mwana Fa na AY wanatarajiwa kuondoka next week ya wiki ijayo kwenda Ulaya kwenye nchi za Finland,Holland,Denmark,Norway,Italy
na Sweden kuwahamasisha watu wasije mjini ambapo watakua huko kwa zaidi ya mwezi mmoja wakipiga show ya Hip hop ya kutakata...

Kila la kheri wana,Mpeni hi 'PWEZA WA UJERUMANI' mkikutana nae,nasikia yu waishi huko!!!



Wednesday, July 7, 2010

DUH...REGGAE INAPOKUTANA NA BOLINGO!!!

Mkali toka Kenya,Wyre amepiga collabo na Mwanamuziki Mkali wa KwasaKwasa toka Congo DRC,Kanda Bongo Man.
Wyre na Bongoman walikutana nchini Sudan kwenye tamasha la Miss Malaika na Bongo Man kuzimia show ya Wyre na kumuomba wapige collabo...Wyre ameshapeleka "Vocal" zake nchini London kwa Producer wa Kanda Bongo Man na tunasubiri mating'a yawe tayari ili mpango mzima uwekwe hadharani...Duh reggae inapokutana na bolingo!!!

Thursday, July 1, 2010

SUGU KUGOMBEA UBUNGE!

Kalapina-Udiwani,Kinondoni-CUF

Nakaaya-Ubunge,Arusha-CHADEMA

Sugu-Ubunge,Mbeya Mjini-CHADEMA

Mkongwe wa Hip Hop Tanzania,Joseph Mbilinyi AKA Sugu ambaye amejinga na CHADEMA hivi karibuni,ametangaza nia yake ya kugombea Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA,jimbo la Mbeya mjini.


Kwa sasa Mheshimiwa mtarajiwa yuko Mkoani Mbeya akiwa kwenye mchakato wa kurudisha fomu baada ya kupata ridhaa ya chama chake...Sugu anaungana na wasanii wengine toka Tanzania kama Kalama Masoud AKA Kalapina anatakayegombea Udiwani jimbo la Kinondoni-DSM kupitia chama cha CUF,na Nakaaya Sumary aliyetangaza nia ya kugombea Ubunge mkoani Arusha kwa tiketi ya CHADEMA...Hatutauza kura zetu....ila Kila la Kheri waheshimiwa watarajiwa!