.

Friday, December 18, 2009

MR II KWENYE POWER JAMS EAST AFRICA RADIO.

Mkesha wa x-mass ndio atazinduwa albam yake ya VETO Sugu pia ana ndoto za kufunguwa Radio station ambayo itakuwa inacheza muziki wa kizazi kipya tu..!!!

Hapa akifafanuwa kiundani kuhusu uzinduzi wake wa albam yake ya VETO.

Sugu akiwa na Dj Mackey katika kipindi cha Power Jams.

Huu ndio mpango mzima sasa...!!!! Sugu pamoja na Dullah kwenye Power Jams.

Huyu ndio Sam mchizi anakamuwa show ya Power Jams East Afrika Radio.

2 comments:

  1. Nimerejea "home". Heshima kwako Kaka
    Haya nimefurahi kurejea na kubambana na taswira za studio. Wengine huu ndio ULEVI wetu.
    Anyway
    Nimefurahi kusikia mengi kuhusu II na pia kusikiliza na kutazama video yake. Nasikitika kuwa kwa nyimbo nilizosikia sijaona nililotegemea. Ni jambo jema kuwa na "identity" katika muziki wako lakini kuna haja ya kuuboresha. Hata Burning Spear na Everton Blender wanaendelea kupiga miziki kwa namna waliyopiga miongo miwili ma zaidi iliyopita lakini bado wanaboresha kwa namna moja ama nyingine. Style yake imebaki kuwa ileile, utengenezaji wake umezidi kujikita kwenye vyombo visivyo halisi badala ya ala na hilo limemuongezea futi kadhaa katika kaburi la uhalisia.
    Najua atauza kwa kuwa "ana jina" lakini hatadumu kwa kuwa muziki hauna ubora.

    Pia bado nina wasiwasi na MPANGO MZIMA wa kuibadili sanaa ya muziki wa kizazi kipya. Nadhani kunakuwa na "kelele" nyingi katika kufanya BIASHARA ilhali akili za wasanii ni za kituma zaidi.
    Naamini kuna haja ya kuacha KUKURUPUKA kusema tunataka mabadiliko kaika soko na hakimiliki wakati wasanii wenyewe wana akili za usaliti na utumwa. Hawajui kwanini wanafanya muziki na kwanini muziki liwe chaguo lao la maisha waishiyo. Wanaota kuliko kuishi na hiyo ni HATARI.
    Blessings Brother
    Tuonane "Next Ijayo"

    ReplyDelete
  2. nashukuru kaka kwa mchango wako na hii ni changamoto kwa wasanii wote wa hapa nyumbani mungu akuzidishie ndugu na akupe maisha marefu ili uweendelee kutoa changamoto ambazo zitasaidia kuusukuma mbele huu muziki wetu.

    ReplyDelete

,