.

Thursday, December 31, 2009

MZEE WETU HATUNAE TENA DUNIANI.

Jina la “Simba wa Vita” ndio jina ambalo watu wengi wamekuwa wakilitumia kumtambulisha mzee wetu Rashid Mfaume Kawawa. Mzee wetu ametutoka leo asubuhi katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alipo lazwa tangu jana na inasemekana matatizo ya kisukari ndio yamesababisha kifo chake na kutokana na hilo mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza bendera ya taifa itapepea nusu mlingoti kwa siku saba.

Rashidi Mfaume Kawawa alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza nchini Tanzania na baadaye kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi. Alizaliwa mwaka 1926 katika kijiji cha Matepwende Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Tanzania. Alianza elimu ya msingi huko Liwale - Lindi mnamo 1941 - 1942 na kuendelea na masomo ya sekondari katika shule ya Dar es salaam Secondary School.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amin.

No comments:

Post a Comment

,