WAZIRI KIKWETE: MFUMO MPYA KUWEZESHA WATANZANIA KUPATA FURSA ZA AJIRA NJE
YA NCHI
-
Na Mwandishi Wetu; Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye
Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete, amesema katika mwaka wa...
9 hours ago
Nimerejea "home". Heshima kwako Kaka
ReplyDeleteHaya nimefurahi kurejea na kubambana na taswira za studio. Wengine huu ndio ULEVI wetu.
Anyway
Nimefurahi kusikia mengi kuhusu II na pia kusikiliza na kutazama video yake. Nasikitika kuwa kwa nyimbo nilizosikia sijaona nililotegemea. Ni jambo jema kuwa na "identity" katika muziki wako lakini kuna haja ya kuuboresha. Hata Burning Spear na Everton Blender wanaendelea kupiga miziki kwa namna waliyopiga miongo miwili ma zaidi iliyopita lakini bado wanaboresha kwa namna moja ama nyingine. Style yake imebaki kuwa ileile, utengenezaji wake umezidi kujikita kwenye vyombo visivyo halisi badala ya ala na hilo limemuongezea futi kadhaa katika kaburi la uhalisia.
Najua atauza kwa kuwa "ana jina" lakini hatadumu kwa kuwa muziki hauna ubora.
Pia bado nina wasiwasi na MPANGO MZIMA wa kuibadili sanaa ya muziki wa kizazi kipya. Nadhani kunakuwa na "kelele" nyingi katika kufanya BIASHARA ilhali akili za wasanii ni za kituma zaidi.
Naamini kuna haja ya kuacha KUKURUPUKA kusema tunataka mabadiliko kaika soko na hakimiliki wakati wasanii wenyewe wana akili za usaliti na utumwa. Hawajui kwanini wanafanya muziki na kwanini muziki liwe chaguo lao la maisha waishiyo. Wanaota kuliko kuishi na hiyo ni HATARI.
Blessings Brother
Tuonane "Next Ijayo"
nashukuru kaka kwa mchango wako na hii ni changamoto kwa wasanii wote wa hapa nyumbani mungu akuzidishie ndugu na akupe maisha marefu ili uweendelee kutoa changamoto ambazo zitasaidia kuusukuma mbele huu muziki wetu.
ReplyDelete