Kampuni ya simu za mkononi Tigo imeanza mwaka kwa kufurahia kwa pamoja na watoto waishio katika mazingira magumu kutoka vituo mbalimbali vya mkoani dare s salaam kwa dhumuni kupata nafasi ya kujifunza na kutambua mahitaji ya watoto hao katika maisha yao ya kila siku ili kama kampuni inayohudumia jamii kujipanga vyema na kusaidia jamii ya aina hiyo kujikomboa.
Akiongea wakati wa hafla hiyo Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Tigo Jackson Mmbando alisema “Leo tumeamua kusherekea kuanza mwaka na watoto hawa katika sherehe hii tuliyoipa jina la WATOTO WA BABA MMOJA ili kuwapa nafasi watoto hawa kufungua mawazo yao na kutufahamisha wanataka tuwafanyie nini katika mwaka huu wa 2010.
Sisi tuko tayari kujipanga na kuhakikisha jamii hii tunaikomboa kwa kushirikiana na wadau mbali mbali nchini Tanzania kama walivyofanya wasanii wa filamu nchini Tanzania leo tuko naon ili kujua matatizo ya watoto wetu.
Tigo kwa kuanza tumeshafahamu kuwa watoto hawa wanamatatizo makubwa sana kwenye swala zima la malazi! Yaani sehu za kulala hivyo tumeanza kuwapatia mablanketi 200 ili yawakimu kwa kipindi hiki. Pia mwezi januari watoto wanarudi shule hivyo wanaitaji vifaa mablimbali kwaajili ya elimu yao hivyo tumewaletea madaftari, penseli, kalamu, Mikebe ( Compus) tukiwa na dhamira ya kuonyesha kwamba mwaka 2010 kwa kiwango kikubwa tutahudumia watoto kama haya katika sekta ya elimu kwa kiasi kikubwa sana.
Tigo tunawakaribisha wadau mbalimbali wanaotaka kuunga dhamira yetu ya kukuza vipaji na kuwaendeleza kielimu watoto wetu kwa kuwa sisi sote ni WATOTO WA BABA MMOJA.
Kwa upande wake mratibu wa Tamasha hilo Joyce Kiria Nkongo alisema “ Ninaishukuru sana Tigo, Uniliver,NMB Bank, EATV&Radio pamoja na wadhamin binafsi waliojitolea, kwa kutuunga mkono katika dhamira yetu ya kukaa na kufurahi pamoja na WATOTO WA BABA MMOJA, kwetu sisi Bongo Movies ni faraja iliyoje kuona mambo yanaenda kama yalivyopangwa mara baada ya kuungwa mkono na wadau mablimbali nchini pamoja na wasanii wa filamu ambao pia walikuwepo bega kwa bega kuwasaidia na kuwaongoza
“Tayari tumeshatengeneza miundombinu na mikakati ya kutosha na wadhamini wetu, kwamba mwaka 2010 uwe mwaka wa mabadiliko kwa kuwaweka watoto wetu wote katika sehemu hali ya kujitambua kuwa wanaweza na wanahaki katika jamii yetu”alimaliza kusema Joyce Kiria Nkongo
Baadhi ya watoto walio hudhuria tamasha hilo.
Dullah mwakilishi wa EATV katika tamasha hilo akitowa zawadi kwa ajili ya watoto yatima waliokutanishwa siku hiyo, pia makampuni mbali mbali yalitowa zawadi.
Hawa ni watoto kutoka vituo mbali mbali.
Masanja wa comed akichukuwa chakula pamoja na watoto hao.
Bi Mwenda akiwa na watoto waliojitokeza siku hiyo.
Hawa ni baadhi ya wasanii wa filam bongo waliojitokeza kushirikiana na watoto na kulanao pamoja.
Dogo chuwa gwala kwanza alafu twende sawa....!!!
Serikali yaweka mikakati ya suluhu ya wezi katika mitandao
-
Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Slaa
akizungumza na waandishi habari kuhusiana na wahalilfu wa mitaondao,jijini
Dar es Sal...
43 minutes ago
No comments:
Post a Comment
,