The Big Names katika Bongo Flava nchini, Shabani Katwilla ‘Q-Chief’ na Khaleed Mohamed ‘Tid’ hivi karibuni wametoleana maneno ya kashfa kila mmoja akimtuhumu mwenzake kuwa ni mchawi.
Ishu nzima iko hiviiii...juzi kati jijini Dsm, mtangazaji mmoja wa kike wa kituo kimoja cha televisheni aligonga mbili tatu hewani na msanii Q-Chief.
Wakiwa kwenye mahojiano ya laivu, Q-Chilah alisikika akisema kuwa tangu ameacha kufanya kazi na TID mambo yake yamekuwa hayaendi vizuri na kwamba tatizo hilo limekuwa ni la kudumu kwa upande wake.
Q-Chief aliendelea kusema siku moja akiwa katika mishemishe zake alikutana na mama mmoja (hakumtaja jina) aliyemwambia kuwa amelogwa na wasanii wenzake wawili akiwemo TID.
Q-Chief aliendelea kupigia msumari na kusisitiza kuwa, ni kweli amelogwa na wasanii hao na hakuna ubishi.
Kwa upande wa TID alisema kuwa, kauli ya Chilah imemdhalilisha sana hivyo ameamua kwenda kuripoti polisi na kwamba atahakikisha anamshughulikia kadiri ya uwezo wake.
TADB, EXIM KUTOA BILIONI 30 ILI KUWAWEZESHA MITAJI WAKULIMA
-
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB),
Frank Nyabundege (kushoto) akipeana mkono na Afisa Mtendaji Mkuu wa fedha
wa ben...
1 hour ago
Jamani are you still believing this shit? Vijana mnatakiwa kuwa wabunifu katika Game na sio kusingiziana uchawi,
ReplyDeleteBy Strive 4 life