.

Thursday, December 31, 2009

MZEE WETU HATUNAE TENA DUNIANI.

Jina la “Simba wa Vita” ndio jina ambalo watu wengi wamekuwa wakilitumia kumtambulisha mzee wetu Rashid Mfaume Kawawa. Mzee wetu ametutoka leo asubuhi katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alipo lazwa tangu jana na inasemekana matatizo ya kisukari ndio yamesababisha kifo chake na kutokana na hilo mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza bendera ya taifa itapepea nusu mlingoti kwa siku saba.

Rashidi Mfaume Kawawa alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza nchini Tanzania na baadaye kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi. Alizaliwa mwaka 1926 katika kijiji cha Matepwende Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Tanzania. Alianza elimu ya msingi huko Liwale - Lindi mnamo 1941 - 1942 na kuendelea na masomo ya sekondari katika shule ya Dar es salaam Secondary School.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amin.

Sunday, December 27, 2009

JOYCE KIRIA NA WATOTO YATIMA.

Kuna kila sababu ya kulifanya hili ni kukaa nao pamoja ili wasijisikie upweke na wajihisi kuwa wote ni watoto wa baba mmoja, hilo ndio dhumuni kubwa lakufanya tamasha ambalo litawahusisha watoto yatima wote lakini watakutanishwa sehemu moja tu ni katika kituo cha Help Ophrarn Tanzania.

Tamasha hili limeandaliwa na kipindi cha Bongo Movies kinachorusha EATV na mratibu wa tamasha hili ni Joyce Kiria na litafanyika januari mosi pia watoto hao watapata nafasi ya kukutana na mastaa mbali mbali wa movies pamoja na Bongo Flava.

Thursday, December 24, 2009

HIP HOP KING OF STAGE.

Huu mchongo unatokea pande za Kikosi cha mizinga sehemu ambayo Hip Hop inachukuwa nafasi yake.

Jamaa wameandaa tamasha la kumtafuta MC ambaye atavikwa taji lakuwa mfalme wa jukwaa katika muziki huu wa Hip Hop, Mpango mzima utakuwa tarehe moja ya mwaka mpya maeneo ni pale pale viwanja vya COCO BEACH na kiingilio ni buku tano tu na hii itakuwa ni nusu fainali na baada ya mshindi kupatikana siku hiyo ndio fainali yenyewe itatangazwa na mshindi atazawadiwa milioni mbili.

Kala Pina ameniambia sababu ya kufanya hivi ni kurudisha heshima ya muziki wa Hip Hop bongo na kuupa thamani muziki huu.

NAWATAKIA SIKUKUU NJEMA WADAU WOTE..!

Tumekuwa pamoja kwa kipindi chote kwenye Blog yangu ya Mpango Mzima kwenye Planet Bongo ya Radio na Tv na tumeweza kupeana saport kwa mambo mbali mbali.

Sasa tunaanza kusheherekea X- MASS na kuu karibisha mwaka mpya wa 2010, nawaahidi kuwa pamoja na nyie na kuundeleza kupeana taarifa na burudani mbali mbali zinazo husu muziki wetu wa Bongo Flav. NAWAPENDA  SANA NA SIKUU NJEMA.

Friday, December 18, 2009

MR II KWENYE POWER JAMS EAST AFRICA RADIO.

Mkesha wa x-mass ndio atazinduwa albam yake ya VETO Sugu pia ana ndoto za kufunguwa Radio station ambayo itakuwa inacheza muziki wa kizazi kipya tu..!!!

Hapa akifafanuwa kiundani kuhusu uzinduzi wake wa albam yake ya VETO.

Sugu akiwa na Dj Mackey katika kipindi cha Power Jams.

Huu ndio mpango mzima sasa...!!!! Sugu pamoja na Dullah kwenye Power Jams.

Huyu ndio Sam mchizi anakamuwa show ya Power Jams East Afrika Radio.

Monday, December 14, 2009

BOBI WINE ACHOMEWA MOTO HOTEL YAKE.

Msanii nyota Bobi wine inasemekana amepoteza mamilioni ya fedha baada ya watu wasio julikana kumchomea hotel yake ambayo anatarajia kuizinduwa mwishoni mwa mwaka huu jijini kampala.

Watu hao walimuharibia baadhi ya maeneo ya hotel yake hiyo na pia kufanikiwa kuchoma sehemu ya kuuzia vinywaji aliyoipa jina la 'Kassim Ouma'.

Friday, December 11, 2009

G5 CLICK ONLINE MUSIC STORE


Kama ilivyotangazwa na G5 CLICK kupitia CLOUDS FM wakati wa interview kwenye kipindi cha XXL (Extra Extra Large), G5 CLICK ENTERTAINMENT COMPANY itaanza kuuza na kusambaza Bongo music, movies na videos za muziki wa kibongo, Artwork, Ring tones, E-Books na Tickets za events mbalimbali kupitia social network website yake (www.G5click.com) kwa makubaliano na wahusika..

Huduma hii itakua online kwanzia januari 2010 kwenye FACEBOOK, G5CLICK na MY SPACE, watu wataweza kununua miziki na vitu vingine vingi kwenye social networks kwa kutumia ATM CARDS zinazofanya kazi online-mfano. VISA

NDANI YA STORE:

BONGO MUSIC – Singles na Albums

E-BOOKS – hivi ni vitabu ambavyo vipo kwenye mfumo wa PDF

ARTWORK – Artist wallpapers, Picha, covers, logos n.k

RINGTONES – Mp3, Mono na Polly tones

TICKETS – Event tickets (Parties, shows, Donations)

MOVIE ZA KIBONGO NA MUSIC


KAMA UNATAKA KUSHIRIKISHWA KWENYE PROJECT HII

TAFADHALI WASILIANA NA SISI KUPITIA:

Email: info@g5click.com ;

Phone: +255-714-204490 or +255-713-889878

Web: www.G5click.com

THANK YOU ALL FOR SUPPORTING G5 CLICK ENTERTAINMENT

By G5 CLICK ENTERTAINME

Q CHILLAH NA TID NA ZENGWE LA UCHAWI.

The Big Names katika Bongo Flava nchini, Shabani Katwilla ‘Q-Chief’ na Khaleed Mohamed ‘Tid’ hivi karibuni wametoleana maneno ya kashfa kila mmoja akimtuhumu mwenzake kuwa ni mchawi.

Ishu nzima iko hiviiii...juzi kati jijini Dsm, mtangazaji mmoja wa kike wa kituo kimoja cha televisheni aligonga mbili tatu hewani na msanii Q-Chief.


Wakiwa kwenye mahojiano ya laivu, Q-Chilah alisikika akisema kuwa tangu ameacha kufanya kazi na TID mambo yake yamekuwa hayaendi vizuri na kwamba tatizo hilo limekuwa ni la kudumu kwa upande wake.


Q-Chief aliendelea kusema siku moja akiwa katika mishemishe zake alikutana na mama mmoja (hakumtaja jina) aliyemwambia kuwa amelogwa na wasanii wenzake wawili akiwemo TID.


Q-Chief aliendelea kupigia msumari na kusisitiza kuwa, ni kweli amelogwa na wasanii hao na hakuna ubishi.

Kwa upande wa TID alisema kuwa, kauli ya Chilah imemdhalilisha sana hivyo ameamua kwenda kuripoti polisi na kwamba atahakikisha anamshughulikia kadiri ya uwezo wake.

Thursday, December 10, 2009

WANA WALIKUWA WAKUTOSHA UCKU WA PWAA

Si unajuwa vi2 vizuri lazima viende na mambo mazuri hivyo sasa.

Pozi za hawa jamaa kama naziomba hivi....!!!

Sara na Shydel

Romy, Shydel, Sara na Dullah.

Romy
Planet Bongo ilikuwepo kuhakikisha hakuna kinachopita bila kuhusishwa.

Izzo b, Adam na Quick Rocka.

Dunga naye ndani katika usiku wa Pwaa.

Huu ndio MPANGO MZIMA...!!!!

Dominick Nyalifa, Dunga na Ay.

UCKU WA PWAA MOVENPICK..

Kutunza pia ilikuwepo ukihisi burudani imekuhusu basiiii mpango mzima..

Pia kulikuwa na nafasi ya kusikiliza ngoma zilizomo kwenye albam yake..

Huyu ni Luch Producer ambaye anafanya kazi na Cpwaaa.. alipata na fasi ya kupiga domo kidogo.



Huyu ni mama yke Cpwaa naye alikuwepo kumpa taf mtoto wake.


Jamani eeeh...!!! huyu ndio bi mkubwa kama mlikuwa hamjui ndio hivyo sasa.

Wednesday, December 9, 2009

BAADA YA KUJITOA RACKAS MKWAJU UKAFATA..

Mchizi alikuwa ni kiongozi wa kundi la Rackas ambapoa kwa sasa hayupo tena. Moracka ameingia Fish Crub kwa Lamar kutengeneza pini yake baada ya kuachana na kundi lake, na kwa sasa mzigo upo tayari sikiliza East Afrika Radio juma mosi hii katika Planet Bongo saa 4 asubuhi hadi saa 6 mchana utapata nafasi ya kuisikia ngoma inaitwa SHE GAT IT.

CPWAA NA SAM KATIKA POWER JAMS..

Cpwaa na Sam katika interview Power jams East Afika Radio.


Hii ilikuwa kabla ya show iliyo fanyika Movenpick Hotel.

Tuesday, December 8, 2009

TUNDA NA MADEE NDANI YA SOUTH AFRICA..!!

Jamaa wanatokea katika kundi la Tip Top Connection ambao wanafanya vizuri katika game la Bongo Flava, hapa namzungumzia Tunda Man pamoja na Madee wamesepa kuelekea South Africa kwa ajili ya kukamuwa show mbili.

Show ya kwanza itakuwa tarehe 11 Captown na ya pili itakuwa tarehe 12 Daban na wanategemea kurudi Bongo juma nne ijayo. Tunda pia alinijuza kuwa jamaa wa Textile Campany ndio wamesababisha mchongo huo.

Monday, December 7, 2009

CYRIL ATIMBA RASMI PANDE ZA TONGWE RECORDS..

Cyril akiwa na Maunda Zoro

Ni kijana mdogo sana ki umri hata umbo pia lakini ni mkubwa sana linapo kuja swala zima la rap, anaitwa Cyril mchizi nyota yake ilianza kung'ara katika mkwaju wake wa Nimerudi ambao ulikamilishwa na Producer Maneke.

Lakini Cyril kwa sasa ametimba rasmi kona za Tongwe Records kwa maana kwamba jamaa amesha sign mkataba chini ya studio hiyo pamoja na J Murder, sooo...!!!! acha 2one mzuka utakuwaje.

Sunday, December 6, 2009

UMAGA AFARIKI DUNIA.

Edward Fatu kutoka visiwa vya Samoa almaarufu kwa jina la UMAGA ambaye ni bingwa wa zamani wa michuano ya mieleka amefariki dunia baada ya kupatwa na shinikizo la damu.

Inasemekana alishikwa na usingizi wakati akitazama televisheni Al-hamis usiku, alikutwa na mkewe masaa kadhaa baadaye akiwa hapumui huku damu zikimtoka puani na kuamua kumkimbiza katika hospitali ya jirani. Umaga amefariki akiwa na umri wa miaka 36.

Thursday, December 3, 2009

JOH MAKINI AWA MAIND WANA WANAOPIGA MAGUMASHI KUPITIA MAUJANJA YAKE...

Mchizi kutoka Arusha Joh Makini amewalalamikia jamaa ambao wanatumia mashairi ya nyimbo zake kutengenezea tshirt , kwa mfano ngoma ya STIM ZIMELIPIWA tayari tshirt zimeshatoka nyingine ni MWAMBA WA KASKAZINI.

Makini anasema tshirt hizo hausiki nazo na anawaomba mashabiki zake kuto kuzinunuwa kwa sababu hazimuingizii chochote, na tayari anashughulikia ishu za kisheria kwa ajili ya hawa jamaa wanaopiga hayo magumashi.


Anasema mchizi mmoja anaitwa Luka wa Sinza kijiweni yeye ni moja kati ya hao wanaofanya hivyo, ameniambia nguo zake atazitowa muda si mrefu na zitapatikana kwenye duka la washkaji wa Maujanja Mwenge.

JUMA MOSI HII MZALENDO PUB...!!!!

CPWAA'S PRE- LAUNCH PARTY NA PLANET BONGO..

Tarehe 8 ya mwezi huu Cpwaa atazinduwa nyimbo mpya, Fashion show ya mavazi yake mapya pamoja na tovuti ya WWW.CPWAA.CO.TZ. bila kusahau documentary ya historia yake ya kimuziki pamoja na BONGE LA SHOW.

Baada ya hilo zitagongwa kopo kutoka kwa Ma DJ wa EAST AFRICA RADIO, kiwanja ni kile kile cha kishuwa ni katika hotel ya MOVENPIC kuanzia saa 3 usiku na kiingilio ni buku kumi na tano tu!! (15,000).

Usiku wa PWAAA! umeletwa kwenu na BRAINSOR MUSIC pamoja na PLANET BONGO ya EAST AFRICA RADIO na TV.

Wednesday, December 2, 2009

MPANGO WA ALBAM UNAZINGUWA.

Unaweza kumuita Abraham Kasembe na kama itakupa tabu basi tumia jina hili Dullayo, mchizi ambaye hivi karibuni alichomwa kisu kwenye mkono wake wa kushoto na watu wasio julikana wakati akitoka katika ukumbia wa starehe.

Mchizi amesema kwa sasa ataendelea kukomaa na single mpaka pale soko la muziki litakapo kaa sawa, Dullayo amesema sababu ya kufanaya hivyo ni kutokana na kutokupata kitu katika albam yake ya kwanza ya IMANI.

MUONEKANO WA COVER YA ALBAM YA VETO YA MR. II


Monday, November 30, 2009

Sunday, November 29, 2009

HAWA NDIO MAPACHA WANNE..

Hapa namzungumzia Chokoraa, Kalala Jr, Chaz Baba pamoja na Jose Mara. Hawa jamaa wanatoka katika band mbali mbali lakini wamegunduwa kwa umoja wao wanaweza wakafanya kitu kitakacho kuwa burudani kwa raia.

Leo ndio utakuwa utambulisho rasmi wa vijana hawa katika ukumbi wa Java Stereon - Kinondoni mlangoni utasalimisha buku tano tu. TID ni moja kati ya wasanii watakao toa taf kwa mapacha hao.

LEO KITANUKISHWA NA MAPACHA WANNE

Thursday, November 26, 2009

TANZANIA & KENYA INDEPENDENCE DAY.

D'BANJI AMESHATIA MAGUU BONGO..

Mwanamuziki Di Banji katikati wa Nigeria amewasili leo mchana kwenye uwamja wa ndege wa mwalimu J.K.Nyerere kwa ndege ya shirika la ndege la Ethiopia Airline.
Mchizi ni moja kati ya wasanii ambao stage itawahusu sana tu juma mosi hii katika viwanja vya Tanganyika Pakers Kawe.

Hii inaitwa Inter-College Special 2009 itakayo sindikizwa na wasanii wengine kutoka Bongo na Kenya, Belle9, Cpwa, Mangwear, Jua kali, Nonini na wengineo wengi kiingilio ni buku tatu jero tu...!!!

UMEJIPANGA NDUGUUUUU....!!!!!!!

Njoo utizame show kali yenye kuunganisha vichwa viwili namzungumzia Fid Q na Mzungu Kichaa, mahali ni pale Russian-Tanzania Cultural Center (Ocean View) kuanzia saa tatu usiku