.

Thursday, May 20, 2010

''MR PREZIDAA''....MSIKILIZENI YEYE SASA!!!!

“Habari yako bana….hop unaendelea poa na kazi, ni hivi ndugu yangu, niliwahi kuambiwa msemo fulani, kuwa katika kila utakalofanya au litakalotokea basi lazima watu wataongea, kwamba ulichofanya sio sahihi. Ikiwa ina maana kuwa watu mara zote hawaridhiki na kile kinachotokeaga.

Nikapewa na mfano pia, kwamba kulikuwa na baba na mtoto na punda wanaenda sehemu ya mbali. Basi yule baba alimpakiza mwanae juu ya punda, huku yeye baba mtu akitembea kwa miguu, watu kuona vile wakasema eti oooh!! baba anamdekeza mwanae, iweje ampakize juu ya punda, basi baba akaamua amshushe mwanae then baba akapanda yeye punda huku mtoto anatembea, pia watu wakasema baba anamtesa mwanae,
baba akaona sio kesi wakapanda wote yule punda, watu pia wakasema tena, kuwa hakuna haki za wanyama?Iweje wamtese yule punda? Iweje punda m1 apandwe na watu wawili? Basi baba alichoamua ni yeye na mwanae kushuka na kutembea kwa miguu huku punda akitembea mwenyewe, alidhani ndo’ afadhali lakini aaaah waaapi!! watu wakasema tena, etii ooh yule mzee hana akili, hajui kutumia vitendea kazi, yaani punda yupo halafu anatembea kwa miguu….ha ha ha ha ha!!!

Kwanini nimetoa mfano huu? kwa sababu hiyo niliyosema hapo juu kwamba watu lazima wataongea tu!! kwa kila kitakachotokea,LAKINI SIO MARA ZOTE WANAONGEA KIMAKOSA TUU, wakati mwingine matatizo yanaonekana wazi, kwahiyo lazima yaongelewe….BACK IN BUSINESS….. TUZO/TUNZO za kili, naamini TUZO ndio sahihi …nway, zimetolewa juzi kati na waliopata wamepata…aya nawapa hongera zao, maana wametengeneza historia ya maisha ya mziki wao, lakini je kweli wanastahili kupata tuzo hizo? wanastahili kuwepo kama nominees katika hizo categories?

Wanafanya aina hiyo ya mziki ambao wameshindia hiyo tuzo? haya ni maswali ya kujiuliza, siwafahamu waliopo kwenye kamati husika ya tuzo hizi, ila naamini watakuwa na uelewa wa mziki wetu, lakini kwa hili la kutokea kila mwaka linanipa mashaka.Hivi tunawezaje kusema basketball imepiga hatua ikiwa kila ligi, kila mwaka timu zinazoingia fainali ni SAVIO na VIJANA? kikapu kitakuwa hakijakua maana vipawa vipya havionekani? au nyie mnatazama katika nyanja zipi? kama sio hizi za baada ya kazi ngumu lazima utunukiwe tuzo.

Jee kweli havionekani? Na kipi kinasababisha visionekane? na je hilo sio jukumu la hawa waandaaaji wa tuzo hizo?Obviously itakuwa ni jukumu lao, maana kati ya hao waandaaji naamini wapo maproducers, nadhani hata mapresenters na d.j’s wa radio na t.v pia na wadau kwa ujumla wa mziki huu pia…..!! 2009-2010 binafsi naamini kabisa game ya mziki wetu ilibadilika sana, na kutawaliwa na chipukizi, ambao wengi wamefanya vizuri sana kuliko hawa wasanii wengine ambao wapo kwenye game kwa muda mrefu. Izzo b, nikki wa pili, roma, Quick r…., diamond, belle9, lina, barnaba, pipi, amini, na wengineo wengi,

siwezi kuwataja wote na haina maana kuwa kama sijakutaja hapa ndo’ hufai…. lah hasha!!Hayo ni baadhi ya majina yaliyonijia haraka tu, hawa mbona walifanya vizuri na waliweza kusimama bora zaidi…je tunawaingiza kwenye category moja tu ya msanii anaechipukia? hapana…mbona ktk category ya msanii bora wa RnB yupo steve, Belle 9, diamond, A.T, hawa wengi wao ni chipukizi kama sio wote…which means waliweza kufanya vizuri zaidi ya wale waliotangulia kwenye game hii, si ndio?Haya tuangalie na upande mwingine wa shilingi, je tukirudi kwa upande wa wanaofanya mziki wa RAP…

ina maana hawa hawakupata upinzani kutoka kwa upcomingz artists wengineo zaidi ya Quick r….. tu?mbona kila mwaka ni kama nominees ni walewale tu wanajirudia?mziki (rap game)tuseme haikui?wao ndo’ bora kila mwaka kweli? ha ha ha ha ha!! ni Quick r…peke yake ndo aliweza kucompete na hawa watu tu? What about roma? Na je nikki wa 2?Business nae pia? hata kala jeremiah pia?
Au ni vigezo gani vinatazamwa katika hili? Na hao nominees wote au wengi wao wame base kwenye topic moja tu, kujisifu wao ndio wanai-run hii game kuliko wengine, huyu anajiita professional , yule anasema anatuvua kama samaki, huyu nae anatuambia tumpishe, huku anatupigia honi…. pom pom pom pishaaaa. IZ DAT HIP HOP????mtu anasema NINA PESA MINGI MPAKA NATAMANI JITEKA…THEN WATU WAPO KING STONE KAMA JAMAICA….thats hip hop????? vipi kuhusu huyu aliyesema…. MIGOMO YA CHUO KIKUU NAITUPIA JICHO LA TATU…SITETEI MPAKA RUTASHOBORWA AKIWA WAKILI KISUTU…

Kwa tafsiri ya haraka haraka nani anafanya hip hop real kati ya hawa? nani anaongea real? ni kweli ana pesa nyingi kiasi hicho hadi anatamani kujiteka? Nway HIP HOP ina vitu vingi ikiwemo consciousness na free styl pia, pengine yoyote atakayechagua moja wapo kati ya hivyo vitu viwili atakuwa ameitendea haki, so may be wana diserve. Msiseme kuwa siku zote nilikuwa wapi sikuongea, maana maneno hayaozi na ukweli utaendelea kuwepo tu.Sitaki kuliongelea hili la HIP HOP, lakini nitaligusia, wengi wanaamini mziki wa HIP HOP ni ule unaozungumzia REALITY,(maisha halisi),kutetea haki, kutoa elimu, kukosoa nakadhalika, but i-base katika sense na consciousness, lakini tunaona nominees wa categories kama hizo hawahusiani na huo uhalisia wa HIP HOP, mfano halisi kwenye nyimbo zao hizo zilizoshiriki? au HIP HOP ni kuwa na beat ngumu tu? ha ha ha ha ha!!

nway hata wenzetu wa America tunaona katika hili pengine wanasuasua ndomana nasi pia, kwa maana vingi tunavitoa kwao.Mashabiki ambao ndo ‘ wanapiga kura, wengi wao hawafuatilii mziki kwa undani na umakini zaidi, mimi naamini hilo, mfano nitakupa……..”


watakapoona kwenye category ya muandishi bora wa nyimbo ya RAP yupo ROMA na ngoma yake ya MR.RESIDENT na yupo na flani na wimbo wake ambao kimsingi huyo flani amesifia tu pombe na starehe za club, hata kama huo wimbo hauna maana, lakini kwa vile tu huyo msanii flani ana album, ni mkongwe, anajulikana sana na alitamba na ngoma nyingi sana basi utakuta shabiki ana vote kwa huyo msanii flani, pasipo kujua tuzo inataka nini katika hiyo category…tena utamkuta anasema aaaah!!ROMA mtoto wa juzi tu atamuweza huyu flani, huyu mkongwe sana, huyu flani alihit na ngoma yake ile ya………….apo anakumbushia ngoma ya nighteen kweusiiiii….wakati award haitaki nyimbo hiyo…

hicho ndicho mashabiki wengi wanakifanya….. Hivi tujadiliane hili unaposema watu watume sms kumchagua msanii bora wa kitu flan, halafu yule artist akawapanga watu wake wampigie kura na wakampigia kura akashinda, je hapo tutakuwa tumemchagua yeye kama bora au? ok sio asilimia zote za kura hutoka kwa wananchi, je nyie majaji mnaangalia vigezo gani? nafahamu kwenye mkutano wenu kabla ya kuanza kuvote mlitaja vigezo vyenu, lakini bado nina shaka na hilo.


Ili msanii afanye vizuri anatakiwa awe na presentation nzuri, production safi na promotion pia iwe ya nguvu zaidi, lakini kwetu hapa bongo hutokea mara chache sana hivyo vitu kuwa kama vigezo vya kufanya vizuri, itz like hakuna formula inayomfanya mtu akafanya vizuri hapa kwetu, tunaona wasanii wanatoa nyimbo za ajabu ajabu lakini zinaheat, sasa nauliza huo ubora wanaoutazama killi award je ni kwa ajili ya air tym hiyo wanayopata hao wasanii au?kama ndivyo je yule atakayeweza kujifanyia air time ya nguvu kubwa ndio ataibuka mshindi? Pengine mimi sijajua ubora wa nyimbo ni upi?Labda ni midundo iwe mikali na vocal ziwe safi na sound iwe poa halafu humo katikati utupie mashairi yako ya mitindo huru yasiyokuwa na maana katika kiwango cha kutosha…… Sitaki na sipendi mtu anaposema mbona America wanafanya hivi…kwani si wao!!
ok sisi tunacopy kwao lakini isiwe kila kitu jamani, tukishindwa kabisa sawa tuvicopy, lakini tutazame na sehemu ya kuvipaste pia jamani.


Wimbo bora wa mwaka, je ni bora kuanzia tungo, midundo, upangiliaji wa mashairi,sauti,style na vingine muhimu? au ni bora kwa sababu unajulikana sana na watu wanaiimba hadi watoto!!Je huo ndo ubora? na yule ambae hajajulikana wala kusikika sana je yeye siyo bora? Basi ni vema hata majina ya categories yakabadilishwa pia. Labda tuite wimbo uliopigwa sana na vituo vya radio, au club, msiniambie kama kilichobora ndo’ hupigwa, eti kama sio bora kisingepigwa…aaaah waaapi….!!mapepe ya kingwendu au kamongo ya mr.ebbo zilipigwa sana kipindi hicho,….pengine zilikuwa bora, mimi sina comments hapo.

Nafahamu wengi wakipata tuzo hakuna hata mmoja atakayeweza kusema hazipo fair kwa sababu amepata, lakini angekosa najua angefunguka tu, yaani huwezi kumfuata mwalimu wako na kumwambia mwalimu umenipatisha….aaaah waaapi!!! hata siku moja.

So sisi ndio tuna nafasi kubwa ya kuliona hilo. Nafurahi kuona vitengo na wadau mbalimbali wanajitokeza kuanzisha tuzo zao, kwa ushauri tu ni vema zikaboreshwa zaidi ya hizi zilizopo sasa, ili mabadiliko chanya yaweze kuonekana…Kwa ushauri wangu mchanga ningeweza kuwa – advice wanakamati wajipange kuwa na tuzo nyingi na waongeze categories pia…

Kila mtu ana uhuru wa kuongea na kocomment kutokana na hizi tuzo,japo kuwa sio lazima….ila ROMA amezaliwa kukosoa vilivyopinda.

Waliopata tuzo al hamdllh….waliokosa next tym famil-lah ol of ‘em BIG UPS!!!!maisha yanaendelea na mziki unaendelea.....ila ukweli siku zote una tabia ya kushinda…no matter how long will take…..CONSCIOUS FOREVER………….O…N…E”

1 comment:

  1. Unajua wewe umechanganya vitu viwili.. Uhalisia na Hasira,Kuna kitu unatakiwa ufaham kukosa tuzo haina maana wewe sio bora,ilamwenzio anaweza kuwa bora zaidi yako na kamwe usiji judge wacha watu waku judge, Mimi naamini kabisa ni kweli tuzo zina kasoro ingawa siku zote hazikosekani,umezungumzia wasanii wa hip hop kama wa tatu ungetaja tu majina acha majungu dogo umezungumzia fid, joe na chid.
    Sasa tuje kwenye uhalisia,katika nguzo za sanaa kuna kuburudisha pia na kuna uwezekano mkubwa tu kigezo hicho kikampa kura mtu, mfano,kuliko anzia chimbuko la hip hop (marekani)kuna watu kama talib kweli, common,nas na wengine wengi tu hawa ni watu wanaoongea vitu vya msingi na wana heshima yao kwa hilo ila tuzo ya kwanza ya common kapata mwaka 2008,kwenye beef ya Nas na jigga.. Jigga ni street commercial Nas ni street sence na kila mmoja ana nafasi yake ingawa Jigga ni more successful than Nas.Nimezungumza haya kwa kuwa wewe na nyimbo yako ya president ambayo kimsingi umeongea vitu vya msingi sawa ila haina maana eti iipiku danger kisa ni more commercial aah men kama ingekuwa hivyo basi wagosi wangejaza kabati hatuendi hivyo grow up son! Kila mmoja ana nafasi kulingana na upokelewaji na hata promo.. wakati Fif anatoa album na Kanyiz pamoja watu walijua Fif atam-out sale kanye but its not all bout Fif its bout label n promo sometimes.. umezungumzia kuhusu mtu mwenye jina na album yes ni kweli mwenye jina na album ana nafasi kubwa coz yupo masikioni mwa watu sana kuliko wewe mwenye single moja.. weezy is the best emcee alive but wat does he talk n is music...? rubbish innit? Drake ni hit wa 2009 ila legends are gretest of all times... acha upuuzi wa kujiona bora kaza matako fanya kazi za maana inshaalah utapata tuzo give 110% kazizako punch lines na concious za kufa mtu utafanikiwa sio single moja kelee kuliko uwezo, na kama ni hivyo i blv utatoka na album sio? sasa tutaona kama nyimbo zote utaongea sence na hautozungumzia majigambo na ndio maana ya hip hop.

    Mwanaharakati wa Hip Hop
    USA

    ReplyDelete

,