.

Wednesday, June 30, 2010

HEAVY WEIGHT MC....KUPIGA SHOW KWA OBAMA!

Joseph Haule AKA Mwana wa msolopa gazi AKA Mti Mkavu AKA Mc shupavu AKA Heavy Weight MC AKA Mr red carpet AKA Mwanaharakati..(Mhh hiyo yangu) ...Mwezi huu anaanza Hip Hop Tour yake ya kimuziki nchini Marekani.

Na hii itakua ni tour yake ya kwanza kupiga kwa Obama tangu aanze game rasmi zaidi ya miaka 15 iliyopita,na ataanza kuwasha moto tarehe 4 July,Houston-Texas..wana wa kwa Obama watasikia live track kali za Hip Hop kuanzia Chemsha Bongo,Bongo-Dsm,Nikusaidiaje,Zali la mentali,Sauti ya Ghetto,Msilie na hits kibao....Hapo Vipi???..Hapo Sawaaaaaaaaaaaaaaaaaaa...............!

MAMA NA MWANA !

Nazizi Hirji AKA Mama Tafari akiwa na mtoto wake wa kiume,Tafari baada ya kujifungua hivi karibuni....kushoto ni kama shemeji yetu ambaye jina kapuni,au nitamuuliza JahFaray kama kweli ndio huyu shemeji yetu!

SWALI LA KIZUSHI...Je mtoto Tafari nae atakua na DreadLocks kama Nazizi????!...Hongera JahFaray (mzee wa wali nazi) kwa kupata mjomba!!!

Monday, June 28, 2010

BATA ZA MB DOG SASA ZATAFUNIWA UNYAMWEZINI

mb dogg amesafiri kuelekea uingereza kwa ajili ya show ambazo zitachukua takriban wiki tatu. akiwa huko atapafom ktk mij tofaut ukiwepo milton keynes, bss onx bristol, pia birmingham.

pia hakuwaacha bure wabongo amewaachia track yake ambayo iko ktk albam yake ya pili ya akili yangu track inaitwa kilio changu. kwasasa mbdog yuko ktka hatua za kumalizia albam yake ya tatu na soon atatambulisha singo yake mpya ambayo amemaliza kurekodi usiku wa kuamkia tar 25. mbdogg anaashukuru mashabik wake wote wanaomsapot ktk game.

Thursday, June 24, 2010

REST IN PEACE MICHAEL JACKSON!!!

Leo 25 June 2010 imetimia mwaka 1 tangu mfalme wa Pop dunuani,Michael Joseph Jackson aiage dunia akiwa na miaka 50.

Mwana alianguka ghafla akiwa mazoezini akijiandaa na show yake ya "THIS IS IT" iliyokua ifanyike nchini Uingereza na madaktari walisema kutumia kwake madawa ya kutuliza maumivu ndiyo yaliyosababisha kifo chake na kupelekea daktari wake Conrad Murray kuingia matatani.

REST IN PEACE (KING OF POP) MICHAEL JACKSON!

HIVI MLISEMA HASHEEM THABEET MREFU EEENHHH?!!


Hasheem Thabeet,Memphis Grizzliers (urefu Futi 7.3)

Manute Bol akila tizi

Marehemu Manute Bol (urefu Futi 7.7)

Mwana anakwenda kwa jina la Manute Bol,raia wa Sudan aliyekua anacheza basketball ligi ya NBA-Marekani na amemzidi Hasheem Thabeet kwa inchi 4.

Alichezea timu za Washington Bullets,Golden State Warriors,Philadelphia Sixers na Miami Heat kuanzia 1985 na alistaafu 1994 na akafariki dunia June 19,2010

....REST IN PEACE...TOLU!

Monday, June 21, 2010

KAMA UNA MKWANJA...SEMA NA BONTA!

Mwana toka pande za A-Town na kundi la RiverCamp Soldiers,Bonta alipiga show pande za TCC Chang'ombe na kuimba na wana mwanzo-mwisho track yake ya Nauza Kura Yangu...Na kama una mkwanja anauza kura yake si unajia uchaguzi October????!!!

Saturday, June 19, 2010

KAMA VP...WEEKEND NJEMA!!

Halafu kama ni Bataaaa,basi kiainaaaaaaa au vpppp.........MIIIAAAAAA!!!!

NAZIZI AKA MAMA NANILIII!!!!

Nazizi

Mwanadada Nazizi toka Kenya anayeunda kund ila Necessary Noise na Wyre,Pamoja na lile la East Africa Bashment Crewinasemekana amejifungua hivi karibuni baada ya kuolewa kwa siri kwa zaidi ya miaka 2 sasa huku siri hiyo ya kuolewa kwake ilikua inajulikana kwa watu wake wa karibu wa familia tu...!

KILA KHERI SISTEE....MIAAAAAA!

Friday, June 11, 2010

...KAMA VP...TUKUTANE LEO UCKU,KEMPINSKI-LEVEL 8!!!


Lile bata la kufa mtu limerudi tena ndani ya Kempinski,Level 8.
Mpango mzima utamhusu Dj mkali toka Kenya,DJ Pinye na Crew nzima ya EA Radio DJs kuanzia saa 3 ucku itakua After Party ya ufunguzi wa World Cup 2010....!

...BROTHERZ & FLOWERS.....CU THERE....!

HEKAHEKA ZA KOMBE LA DUNIA KUANZA LEO!!!

Shakira akiimba jana wimbo maalum wako Kombe la Dunia 2010,Time For Africa (WakaWaka)

Uwanja wa Orlando ambapo Sherehe za kukaribirisha kombe la dunia zilifanyika jana Soweto

Prezidaa Jacob Zuma wa Sauz akiwa na timu ya South Africa

Michuano ya 19 ya Kombe la Dunia 2010 inaanza leo kwa mara ya kwanza kufanyika barani Afrika nchini Afrika Kusini mpaka July 11,Mtanange unaanza leo kwa wenyeji Sauz kukipiga na Mexico Kwenye dimba la Soccer City mida ya saa 11 jioni.

GOD BLESS TIMU ZA AFRIKA...!

Thursday, June 10, 2010

SWALI LA KIZUSHI!!????

Mwana akimpa hug la nguvu KAKA.

Mwana akisherehekea baada ya kula shavu.

Askari wakiwa kazini....!

.....Usijiulize ilikuaje mpaka mwana Nagar Ally Kombo akaingia uwanjani na kumkumbatia mchezaji Kaka wa Brazil siku walipocheza na Taifa Stars kwenye uwanja wa Taifa wakati askari walikua kazini!!!...............

Wednesday, June 9, 2010

KUNDI JIPYA LA WANAUME!!!!

Kundi jipya la Wanaume!

Kundi jipya liitwalo WANAUME limeundwa kutoka kwenye lile lililokua awali la TMK Wanaume Halisi.

Machizi wanaounda kundi hilo ni Kakaman,Juma Jazz,Mzimu,Rich One,Daz P na A Man na wamesharekodi track 3,Mapenzi kitu gani,Poa tu pamona na Mukide ambazo zitakua hewani hivi karibuni.

Kwasasa kuna makundi 3 ya Wanaume...yaani TMK Wanaume Family inayoongozwa na Mkubwa Fella,Wanaume halisi chini ya Juma Nature na la Wanaume.

.........KILA LA HERI WANAUMEEEEZ...!!!

TUMSIKILIZE HUYU KIJANA SASA....!!!

Twahir AKA Sajna.

All the way toka Mwanza mpaka Dar namleta kwenu kijana Sajna ambaye yuko juu na single yake ya kwanza,IVETA.

Album yake ya kwanza itakua na nyimbo 10 na itakua kitaani baada siku chache zijazo na wana kama Belle 9,Linah,Josefly na wengine kibao wamepata shavu humo ndani.

Mzigo umepitia studio mbalimbali kuanzia Tetemesha Records,AB Records,Music Lab,Mzuka Records na A2P Records chini ya mikono ya ma-producer wakali kama Kid Bway,Benjamin,Duke,Amba na Sam Timba wamenyonga Beats.

....HOPE ITAKUA ALBUM KALI NA WADAU TUISUBIRI TUONEEEEEE!!!!!!!!!

CONCERT YA KUIKARIBISHA KOMBE LA DUNIA KUPIGWA LEO!

Fifa World Cup

K'Naan-Somalia.

John Legend-Marekani.

Angelique Kidjo-Benin.

Hugh Masekela-South Africa.

Shakira-Colombia.

Black Eyed Peas-Marekani.

Wakali kibao toka pembe zote za dunia leo watapiga concert ya kukaribisha michuano ya 19 ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini kwenye uwanja wa Orlando jijini Soweto.

Zaidi ya watu 30,000 wanatarajiwa kuhudhuria Concert hiyo ambayo wanamuziki K'Nann,Shakira,Angelique kidjo,John Legend,mkongwe Hugh Masekela,Black Eyed Peas na wengine kibao watapiga show kali.

Tuesday, June 8, 2010

OLIVER N'GOMA AFARIKI DUNIA!

Marehemu Oliver N'goma AKA Noli.

Enzi za uhai wake akiwa jukwaani!

Mwanamuziki toka Gabon,Oliver N'goma amefariki dunia Jumatatu kwenye hospitali ya Omar Bongo jijini Libraville akiwa na miaka 51 kutokana na matatizo ya figo yaliyokua yanamsumbua kwa muda wa miaka 2.

Oliver N'goma alikua anajulikana kama "African King of Zouk" na nyimbo zake za zouk kama Bane,Adia,Muendu,Icole na nyingine kibao zilitamba afrika na duniani kote na alipiga show yake ya mwisho siku ya Jumapili wakati akizindua kitabu chake kinachohusu maisha yake na muziki kwa ujumla.

...REST IN PEACE,AFRICA KING OF ZOUK.....!!!!


SUGU KUJA NA ANTIVIRUS PROJECT!

Joseph Mbilinyi AKA Sugu

Mkongwe wa Hip Hop-Tanzania,Sugu anakuja na project itakayojulikana kama ANTIVIRUS,itakayohusu mapinduzi na kuwahusu wote wanaojihusisha na kuuhujumu mziki wa kitanzania na kuwarudisha nyuma wasanii wanaodai haki zao.

Antivirus itakua ni mixtape ambapo kila msanii ataingiza topic yake na kuwataja watu wanaohusika ku-felisha harakati zao na mixtape hiyo itagaiwa bure kwa Watanzania.

Antivirus mixtape itasajiliwa COSOTA na Vol 1 itakua na Part 1 mpaka 10 na itakua na nyimbo 16 ndani yake...halafu itafuata Vol 2,huku wasanii Dudubaya,Afande Sele,G-Solo na wengine kibao watapata shavu kuingiza mavoco yao,huku project nzima ikisimamiwa na Mkoloni,Danny Msimamo pamoja na Dotto Maujanja.


Saturday, June 5, 2010

BREAKING NEWS...BWAN' CHUCHU HATUNAYE TENA!

Marehemu Chuchu kulia akiwa na Kingwendu!

Yussuf Ahmed Alley AKA Bwan Chuchu amefariki dunia jijini Nairobi-Kenya.

Chuchu alijipatia umaarufu mkubwa miaka ya mwanzoni mwa 2000 na bendi yake ya Chuchu Sound,iliyokua na wakali kama Mao Santiago,Omary Mkali,Waziri Sonyo,marehemu Gabby Katanga na wengine kibao,hasa na kibwagizo cha ''EEH..KWAHERI'' kwenye miondoko ya mduara.

Na mpaka anafariki alikua anamiliki studio ya Heartbeat Records na kituo cha redio cha Chuchu FM vyote vipo kisiwani Zanzibar,na haijajulikana mara moja chanzo cha kifo chake.

Msiba upo Kisima Majongoo na Mazishi yanafanyika kwenye makaburi ya MwanaKwerekwe leo saa 10,kisiwani Zanzibar.

MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI...AMIN!

PICHA KWA HISANI YA CRUSHZENJIFM.BLOGSPOT.COM

***************************
........http://ujazo.blogspot.com............1 Luv..Keep It real!!!

Friday, June 4, 2010

G5 CLICK.COM


DON CARLOS APIGA SHOW KALI KENYA

Don Carlos akikamua jukwaani!

Ma-Jah wa kenya mzuka umepanda!

Nyomi la kufa mtu...!

Don McCarlos au Don Carlos gwiji wa Reggae toka Jamaica ambaye pia ni muasisi wa Black Uhuru amepiga show kali na ya kukumbukwa nchini Kenya mwisho mwa mwezi uliopita.

Tamasha lilikua linaitwa SawaSawa na lilifanyika kwenye viwanja vya Kasarani na nyomi lilikua la kufa mtu...kuhusu kitu cha arusha...hapo no comment!

Thursday, June 3, 2010

MHHH!...ZIMBABWE 0 - BRAZIL 3

Timu ya taifa ya Brazil ''El Selecao" imeifunga timu ya taifa ya Zimbabwe ''The Warriors'' kwa goli 3 bila mbele ya watazamaji 60,000 kwenye uwanja wa taifa jijini Harare kwa magoli ya Bastos dk. 41,Robinho dk. 44 na Elano dk,56.

Tarehe 7 June,Brazil itakua nchini Tanzania kucheza na Timu ya taifa ya Tanzania ''Taifa Stars" kwenye uwanja wa Taifa,Dsm

BEBE COOL AZINGUA ULAYA!

Bebe Cool na Wife wake Zuena

Bebe Cool toka Uganda jana karibu achezee kichapo toka kwa machizi wa nchini Denmark baada kuwasemea mbovu baada ya kupiga show akiwa kwenye wheelchair,kwanza alim-diss mchizi mmoja kuwa ni mjinga wala hana passport ya kuishi nchini humo na kufanya fans kum-mind na kudai kama vp kuwa yeye ni superstar wala hawawezi kumpiga.

Timbwili ilibidi liingiliwe na Polisi ili kurudisha hali ya amani na mwana anatarajiwa kuendelea kupiga show kesho tar 4 nchini Holland na tar 5 June nchini Ujerumani.

HEBU TUJIULIZE!!!

Tanzania tangu tumeanza mishemishe za muziki wa kizazi kipya ni kama miaka 20 sasa,wanamuziki toka Tanzania haijalishi unafanya aina gani ya muziki,aidha Bongo Flava,Hip Hop,Muziki wa Dansi,Kwaya ...NK.
Je tuliwahi kufikiria kuwa utandawazi umeifanya dunia kwa sasa kugeuka kijiji? Na kwa dhana hiyo hebu tujiulize maswali yafuatayo...
1. Je wasanii wangapi toka Tanzania wana website zao binafsi?

2.Na kama hawana,je wataweza vipi kijitangaza kazi zao kimataifa?

3.Mbali na kuwa na website labda inaweza kuwa ngumu kwao,Je hata uki-Google utapata habari za msanii husika kama zinavyopatikana za wasanii wengine duniani?


4. Kama nahitaji kujua habari za msanii wa hapa nyumbani nitazipataje kama tu sijuani nae wala sina namba yake ya simu?

5.Hivi kwa vyanzo hivi vichache vya habari hasa Blogs tulizonazo,Je ni asilimia kubwa ya wasanii wanavitumia kwa ajili ya kutuma habari na update zao ili fans wao wajue kinachoendelea?

6.Mwisho kama wewe msanii hufanyi moja kati ya haya,Je tunategemea hizi juhudi za kufanya muziki wetu utambulike kimataifa,zitawezekana? Na vipi kuhusu kupata show za nje kama tu simu yako not reachable,huyo promota atakupataje wakati huna hata website yako binafsi?

...Ni hayo tu wadau...naomba majibu yenu!!!!

BONGO TO THE NEXT LEVEL!

Mwana anaitwa Proveli Paragon Hip Hop Artist,Mbongo ambaye alianzia mishemishe za muziki nchini Canada zaidi ya miaka 10 sasa amerudi Bongo na Target yake ni kuunganisha Hip Hop ya Tanzania na ya Canada.Kwani mwana ameshafungua show za wakali kama Flo-Rida,Lil Wayne,NAS walipokwenda nchini Canada na wengine kibao.

Mwana ana track kibao zinazoshika kama Dirty Lover,na track mpya Slow Burning ambazo amerekodi nchini Canada,na sasa yuko kwenye mikakati ya kumalizia Recording Studio yake pande za Makongo Juu itakayoitwa PEPONI RECORDS.

Wednesday, June 2, 2010

AY ANG'AZA TUNZO ZA MUSEKE.

Kidume cha mzee Yesaya kinazidi kufanya poa katika huu ulimwengu wa muziki na kuisimamisha dede bendera ya Tanzania... Hapa namzungumzia kijana anayemiliki kampuni ya rubudani inayoitwa Unit Entertainment... Ni A.Y

Ameshinda tunzo ya East African song of the year kupitia wimbo wa LEO katika tunzo za Museke za Ghana.. Na leo hii anaenda Kampala kwa ajili ya kufanya show katika fainali za Pilsner Djs Spinning.

"Napenda kuwashukuru mafans wote walioni support kwa kunitakia kheri na kunipigia kura katika tunzo za Ghana zijulikanazo kwa jinala la Museke na kufanikiwa kushinda.. na ushindi huu si wa A.Y peke yake bali ni ushindi wa Tanzania, Mashabiki wa A.Y na mashabiki wa muziki kiujumla.. Nafanya kazi sana , mnanipa support kubwa na mafanikio bado hatujayafikia so mo faya" Hayo ni maneno ya A.Y

Tuesday, June 1, 2010

BREAKING NEWS..McCARTHY AACHWA!!

Mkali Benedict McCarthy ameachwa kwenye kikosi cha wachezaji 23 wa South Africa kitakachoshiriki kombe la Dunia na Kocha wake Carlos Alberto Pereira.