.

Saturday, June 5, 2010

BREAKING NEWS...BWAN' CHUCHU HATUNAYE TENA!

Marehemu Chuchu kulia akiwa na Kingwendu!

Yussuf Ahmed Alley AKA Bwan Chuchu amefariki dunia jijini Nairobi-Kenya.

Chuchu alijipatia umaarufu mkubwa miaka ya mwanzoni mwa 2000 na bendi yake ya Chuchu Sound,iliyokua na wakali kama Mao Santiago,Omary Mkali,Waziri Sonyo,marehemu Gabby Katanga na wengine kibao,hasa na kibwagizo cha ''EEH..KWAHERI'' kwenye miondoko ya mduara.

Na mpaka anafariki alikua anamiliki studio ya Heartbeat Records na kituo cha redio cha Chuchu FM vyote vipo kisiwani Zanzibar,na haijajulikana mara moja chanzo cha kifo chake.

Msiba upo Kisima Majongoo na Mazishi yanafanyika kwenye makaburi ya MwanaKwerekwe leo saa 10,kisiwani Zanzibar.

MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI...AMIN!

PICHA KWA HISANI YA CRUSHZENJIFM.BLOGSPOT.COM

***************************
........http://ujazo.blogspot.com............1 Luv..Keep It real!!!

1 comment:

  1. Thanks for the information....nimeiiba story hii na kuipaste on my blog(http://ujazo.blogspot.com/))kazi njema na maisha yaendelee kama kawaida...

    ReplyDelete

,