.

Thursday, June 3, 2010

HEBU TUJIULIZE!!!

Tanzania tangu tumeanza mishemishe za muziki wa kizazi kipya ni kama miaka 20 sasa,wanamuziki toka Tanzania haijalishi unafanya aina gani ya muziki,aidha Bongo Flava,Hip Hop,Muziki wa Dansi,Kwaya ...NK.
Je tuliwahi kufikiria kuwa utandawazi umeifanya dunia kwa sasa kugeuka kijiji? Na kwa dhana hiyo hebu tujiulize maswali yafuatayo...
1. Je wasanii wangapi toka Tanzania wana website zao binafsi?

2.Na kama hawana,je wataweza vipi kijitangaza kazi zao kimataifa?

3.Mbali na kuwa na website labda inaweza kuwa ngumu kwao,Je hata uki-Google utapata habari za msanii husika kama zinavyopatikana za wasanii wengine duniani?


4. Kama nahitaji kujua habari za msanii wa hapa nyumbani nitazipataje kama tu sijuani nae wala sina namba yake ya simu?

5.Hivi kwa vyanzo hivi vichache vya habari hasa Blogs tulizonazo,Je ni asilimia kubwa ya wasanii wanavitumia kwa ajili ya kutuma habari na update zao ili fans wao wajue kinachoendelea?

6.Mwisho kama wewe msanii hufanyi moja kati ya haya,Je tunategemea hizi juhudi za kufanya muziki wetu utambulike kimataifa,zitawezekana? Na vipi kuhusu kupata show za nje kama tu simu yako not reachable,huyo promota atakupataje wakati huna hata website yako binafsi?

...Ni hayo tu wadau...naomba majibu yenu!!!!

No comments:

Post a Comment

,