.

Tuesday, June 8, 2010

SUGU KUJA NA ANTIVIRUS PROJECT!

Joseph Mbilinyi AKA Sugu

Mkongwe wa Hip Hop-Tanzania,Sugu anakuja na project itakayojulikana kama ANTIVIRUS,itakayohusu mapinduzi na kuwahusu wote wanaojihusisha na kuuhujumu mziki wa kitanzania na kuwarudisha nyuma wasanii wanaodai haki zao.

Antivirus itakua ni mixtape ambapo kila msanii ataingiza topic yake na kuwataja watu wanaohusika ku-felisha harakati zao na mixtape hiyo itagaiwa bure kwa Watanzania.

Antivirus mixtape itasajiliwa COSOTA na Vol 1 itakua na Part 1 mpaka 10 na itakua na nyimbo 16 ndani yake...halafu itafuata Vol 2,huku wasanii Dudubaya,Afande Sele,G-Solo na wengine kibao watapata shavu kuingiza mavoco yao,huku project nzima ikisimamiwa na Mkoloni,Danny Msimamo pamoja na Dotto Maujanja.


No comments:

Post a Comment

,