.

Monday, January 25, 2010

DAZ AMETOWA SOMO KWA WASANII WA BONGO FLAVA.

Mchiz ambaye anafanya muziki wa kizazi kipya David Jacob ‘Daz Baba’ ametoa onyo kali kwa wasanii watakaotumiwa na vyama vya siasa katika kampeni za uchaguzi mkuu kuepuka kuwa chanzo cha kuchochea vurugu kwa nchi yetu kwa kutunga nyimbo za kampeni zinazojenga chuki kwa vyama vingine ama kwa Watanzania.

Daz alitoa wito kwa Watanzania kuepuka kuingizwa katika uhasama na wasanii wasiopenda amani ambao wataingia mikataba na baadhi ya vyama vya siasa kwa ajili ya kuhamasisha chuki baina yao na vyama vingine ama kundi la watu fulani.


kipindi cha kampeni kimefika na baadhi ya vyama vimekuwa vikipenda kuwatumia sana wasanii katika kampeni ila bado wasanii wasikubali kutumiwa kuvuruga amani ama kutumika bila kuwepo maslahi kwao.

No comments:

Post a Comment

,