.

Thursday, January 7, 2010

SHAVU KWA NAVIO.

Msanii Navio wa nchini Uganda amekuwa masanii wa saba nchini humo kuingia mkataba na kusainiwa na kampuni ya Ugandan Talent 256.
Navio ambaye jina lake kamili ni Daniel Kigozi ameizungumzia hatua hiyo kuwa ni mwanzo mzuri wa kupata mafanikio katika fani yake ya muziki.

Kampuni hiyo mpaka sasa ina wasanii wengine wakiwemo Blue 3, Michael Ross, Tonix, Richie na Atlas na tayari imewasaidia kupata nafasi ya kufanya maonyesho nje ya nchi.

Pia kampuni hiyo imefanikiwa kuwaleta wasanii kadhaa wakubwa duniani kufanya maonyesho Afrika Mashariki, wakiwemo Beenie Man, Montell Jordan, Elephant Man na Collie Buddz.

No comments:

Post a Comment

,