.

Sunday, January 31, 2010

LUTEN KALAMA OUT TMK HALISI..

Mchiz ambaye mwanzo alikuwa katika kundi la Gangwe Mob na baadaye kijiunga na kundi la TMK WANAUME kabla ya kusambaratika na kuhama na Juma Nature sasa na amesepa tena na hayupo tena na kundi hilo.

Sababu kubwa iliyomfanya Luten kusepa ni mkwanja anasema haoni faida ya kuwa na kundi kwa sababu hakuna chochote anacho kipata sasa imebidi afanye kazi mwenyewe labda mafanikio yatakuja kwa njia hiyo.

WADAU NA MSHUKURU MUNGU HALI YANGU SASA INARIDHISHA KIDOGO

Tangu siku ya Alhamis hali yangu kiafya ilikuwa haipo sawa na kikubwa zaidi ni malaria, baada ya kujihisi tofauti nikagunduwa malaria inaninyemelea ikanibidi ni wahi hospital na baada ya kupima nikakutwa na wadudu wawili.

ikabidi niazishiwe doz ya malaria na kwa sasa nashukuru Mungu naendelea vizuri, pia nitakuwa mchoyo wa shukrani kama sinto washukuru wale wote ambao walikuwa wakinipa pole katika kipindi hiko cha kuumwa ni Dj Choka, Moracka, Mangwea, Rado, Barut Boy, Dj AD na familia yangu nawashukuru sana na mungu awazidishie ASANTEN SANA.

Tuesday, January 26, 2010

ISIAKA MC YUPO IRINGA..

Isiaka (aliye inama) na mchiz wake.
Isiaka Zayumba a.k.a Isiaka mc mchiz zamani alikuwa anafanya muziki wa kizazi kipya lakini kwa sasa yupo iringa kwaajili ya kutafuta maisha kwa style nyingine ya utangazaji ambapo anapiga mzigo katika radio ya Country fm.. mchiz kaona dah.... chede za radio pekee kama sio ishu hivi... soo.. ameamuwa kugeukia katika upande mwingine wa pili wa kutengeneza beats katika studio ya Timamu Records.

HAYA MA BISHOSTI KAZI KWENU..

Si mnasema mnaenda na wakati haya sasa...!!!! Hicho kiatu kwa mbele kinamuundo kama wa gari aina ya OPEL.

AFANDE SELE AMETOA CHEUPE KWA JOH MAKINI NA MADEE..

Mchizi kutokea Morogoro Afande sele ameamuwa kuweka wazi hisia zake kuhusu mchiz kutoka Arusha Joh Makini pamoja na Rais wa Manzese Madee. Afande Sele ametowa hisia zake hizo wakati alipokuwa anauzungumzia wimbo wake mpya wa KINGDOM wimbo ambao amezungumzia mambo mbali mbali yanayo husu muziki huu. Afande aliuzungumzia wimbo wa Joh Makin wa "NIAJE NIVIP" kuwa ni wimbo ambao mchiz ametumia maneno ya kudhalilisha, wanawake wa nchi masikini kama Tanzania ambao ni mashabiki wa hip hop na Bongo flav.

Alitolea mfano katika ubeti wa Nik wa Pili katika huo wimbo kuwa "washindi wa tuzo za kili wanavuja kama fistula, jipime kama una tundu nyuma ya kaptula" anasema "huwo ni ubeti unao wazalilisha wanawake, hawa wagonjwa wa fistula hawakupenda kuwa hivyo" alisema Afande.


Kwa upande wa Madee alipaka mbayaa.. kuhusu Madee na kusema kuwa "huwezi kujiita Rais wa manzese wakati unaimba matusi, Rais gani unatukana hovyo, Rais gani huna ofisi..?? Wewe unajiita Rais lakini unaimba vitu vya kipuuzi ambavyo mtu akisikia anaona kabisa kuwa ulikurupuka" hayo ni maneno ya Afande Sele kwa Madee.

Mwisho Afande Sele alitoa ushauri kwa wasanii wote kuwa wasiige mambo ya ki- Marekani ambayo hayawasaidii, na si kila kitu anacho fanya msanii wa Marekani sisi tukifanye tubadilike"

Monday, January 25, 2010

CHAMELEONE KUIWAKILISHA AFRIKA MASHARIKI KOMBE LA DUNIA..

Msanii wa nchini Uganda, Jose Chameleone amechaguliwa kuwa mmoja kati ya wasanii watakao toa burudani siku ya ufunguzi wa wa kombe la dunia nchini Afrika Kusini.

Chameleone ambaye atawakilisha Afrika mashariki mwezi june, inasemekana ameingia mkataba wa dola 50,000 kwa ajili ya safari hiyo Afrika Kusini.

MUDA SIO MREFU TUTAMUITA MAMA NANILIU..

Msanii nyota maunda zorro anaujauzito, bishosti huyo ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu anatarajia kujifunguwa mwishoni mwa mwezi wa tatu mwaka huu.
Hata hivyo maunda hajamuweka wazi kidume chenyee ujauzito huo, haya kila la kheri Maunda.

DAZ AMETOWA SOMO KWA WASANII WA BONGO FLAVA.

Mchiz ambaye anafanya muziki wa kizazi kipya David Jacob ‘Daz Baba’ ametoa onyo kali kwa wasanii watakaotumiwa na vyama vya siasa katika kampeni za uchaguzi mkuu kuepuka kuwa chanzo cha kuchochea vurugu kwa nchi yetu kwa kutunga nyimbo za kampeni zinazojenga chuki kwa vyama vingine ama kwa Watanzania.

Daz alitoa wito kwa Watanzania kuepuka kuingizwa katika uhasama na wasanii wasiopenda amani ambao wataingia mikataba na baadhi ya vyama vya siasa kwa ajili ya kuhamasisha chuki baina yao na vyama vingine ama kundi la watu fulani.


kipindi cha kampeni kimefika na baadhi ya vyama vimekuwa vikipenda kuwatumia sana wasanii katika kampeni ila bado wasanii wasikubali kutumiwa kuvuruga amani ama kutumika bila kuwepo maslahi kwao.

HAPA NI MWENDO WA NYAGI TU....!!!

Majingle akiwa na Linex baada ya pilika pilika za hapa na pale mwisho wa siku unajituliza na konyagi baridiiiiiiiiiii.....!!!!!

Friday, January 22, 2010

MTAZAMO WA BANANA KWA MWAKA HUU..

Msanii nyota Tanzania, Banana Zorro amewaasa wasanii wenzake kuwa mwaka huu wa 2010, wajipange vilivyo ili walete vitu vipya kwa mashabiki wao.
Banana ameendelea kusema kuwa kwa sasa wasanii wanaotegemea waingie studio warekodi alafu mwisho wa siku waingie sokoni kuuza mwaka wa 2010 utakuwa mgumu sana kwao, kwa vile mazingira hayaonyeshi dalili yoyote ya mafanikio kwao.

HAYA SASA HUU NI WAKATI WA KUJIPANGA KWA WASANII WETU ILI KUTIMIZA MALENGO.

NIRVANA YA EATV SASA MPANGO MZIMA..

NIRVANA ni kipindi kinacho rushwa na EATV na kwa muda mrefu kilikuwa hakipo hewani kwa ajili ya kukiboresha zaidi na kwa sasa kipo pao tayari kwa kurudi tena hewani kikiwa na mtazamo mpya na watangazaji wapya. USIKOSE NI KILA JUMA NNE SAA MOJA KAMILI USIKU EATV PEKE..

Wednesday, January 20, 2010

KITABU CHA BONGO FLAVA KINATIMBA KITAANI..

G Sollo ni moja kati ya wanamuziki wa hip hop bongo na pia ndio mwaandishi wa kitabu kipya kinachohusu ishu za bongo flava, Kitabu hicho kinaitwa HARAKATI ZA BONGO FLAVA NA MAPINDUZI.

G Sollo ameamuwa kuandika kitabu hicho ili kuelezea athali za muziki huu wa bongo flava pamoja na faida zake kiujumla tofauti na hilo kitabu hicho pia kina barua maalum ambayo ameamuandikia mh. Rais.

G Sollo ameniambia kitabu chake kipo katika matayarisho ya mwisho na tarehe tano ya mwezi wa pili kitakuwa mtaani kwa ajili ya kuwapa raia nafasi ya kuufahamu vizuri muziki huu wa bongo flava

Tuesday, January 19, 2010

DIAMOND RASMI KITAANI SIKU YA VALENTINE..

Bwa ndogo ambaye amefanya vizuri kwa kipindi hiki na song lake la KAMWAMBIE anaachia Albam yake rasmi siku ya Valentine, hii itakuwa tarehe 14/02/2010 hapa namzungumzia Naseeb abdul Juma a.k.a Diamond.

Albam hiyo yenye nyimbo kumi na mbili inaitwa KAMWAMBIE, wasanii walio pata shavu la kuwemo katika albam hiyo ni pamoja na Ngwair, Hemedy, Mabovu, Blue, Fatma na wasanii chipukizi.
Mzigo umekamilika katika studio tofauti ikiwemo Sharobaro Rec, 41 Rec, Fish Crub Rec, pamoja na Sei Rec. Jukumo lote la kusambaza albam hiyo imeachiwa kampuni ya FM WASAMAZAJI.

TING'A KALI NAMBA MOJA KWA VIJANA..


HUU NDIO MPANGO MZIMA...!!!

Monday, January 18, 2010

COVER YA FILAM YA LOLEZA..


Hizo ni cover za filam mpya ya LOLEZA ambayo nilikuhabarisha ipo njiani kuja ambayo imetengenezwa na kampuni ya Chapakazi Film ambayo mtu mzima Adil ndio kamaaaaa.... MPANGO MZIMA.. very soon...





MNUSO WA IPP NA WATU WENYE ULEMAVU..

Oyaaaa... zije ngapi huko...????
Wafanyakazi wa IPP ndio waliokuwa wahudumu kwa walemavu walio kuja kupata chakula cha mchana.

Huyu ni Patrick Nyembera 5 sport kugawa chakula kulimuhusu pia.

Sam Misago wa Power Jam East Africa Radio.

Steav Kafire akiwa tayari kugawa chakula kwa wahusika.
Ni wakati wa mpunga.
Mwenyekiti wa makampuni ya IPP ndiye alikuwa wa kwanza kuanza kugawa chakula kwa walemavu ndio vijana wake wakafatia.
Watu mbali mbali walijitokeza katika mnuso huo Prof Jay, Michuzi na Ay.
Vyombo mbali mbali vya habari vilihusika pia.
Mh. Waziri mkuu Mizengo Pinda ndio alikuwa mgeni rasmi.
Michuzi, Lady Jay Dee, Mwasiti na Marlaw wote walihusika pia.
Huyu ni shabiki wa Diamond alipata nafasi ya kumuona live ikabidi asogee karibu ili kupiga naye story.
Binti Machozi na anko Michuzi.
Tid akiongea na EATV.

Ukumbi wa diamond ulifunga mbaya, walemavu wote walipata nafasi ya kukutana pamoja na kubadilishana mawazo na kupata chakula cha mchana kilicho andaliwa na mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Bw. Reginald Mengi.

Friday, January 15, 2010

VIDEO YA WIMBO WA BATA MARUFUKU BAADHI YA TV ..

Washikaji kutoka visiwani Zanzibar Off side trick wamelala mika kuwa baadhi ya Tv hapa bongo kuzuia kuchezwa kwa video yao ya wimbo wa Bata video ambayo imetengenezwa na kampuni ya Golden hrt ambayo inaogozwa na Abraham.

Wana wasema wamepata taarifa hizo kutoka katika vituo hivyo baadhi vya Tv na kuwaambia kuwa video yao haina maadili mazuri ya ki- Tanzania na huwezi kuitazama kama upo na familia yako, lakini wameniambia kuwa hawajapata taarifa rasmi kutoka kwa vyombo husika kama TCRA kuhusu video hiyo kuchezwa ama la.


Lakini wameamuwa kutengeneza video nyingine ya wimbo huo wa Bata na sasa wapo katika harakati za kukamilisha kichupa hicho kingine.

JULIANA KANYAMOZI NA IRYN NAMUBIRU SASA MPANGO MZIMA..

Inasemekana kuwa wasanii nyota nchini Uganda Juliana Kanyamozi na Iryn Namubiri wanatarajia kukamua katika ngoma moja inayo husu siku ya wapendanao, Valentines Day.

Wawili hao ambao walikuwa hawapatani siku za nyuma, inasemekana kuwa kwa sasa wanaongea na wanatarajia kurecord wimbo huo ambao umeandikwa na Hope Mukasa.

BAADA YA MUDA MREFU CHIDI TENA KIDEONI..

Rappa Chid Benz ambaye anawakilisha kundi la La Familia aka 'NWO' au New World Order yupo mbioni kuachia video za singles zake mpay. Katika video hizo, Chid amewashirikisha wasanii kutoka Kenya na Uganda. Mbali na hapo Chid pia ameandaa project mbali mbali atakazo shirikiana na wasanii kutokea nchini Rwanda na Burundi.

Tuesday, January 12, 2010

SHAVU LINGINE KUTOKA EATV..!!!

Je unajua kwamba Tanzania ni nchi iliyojaliwa kuwa na historia ya sanaa tangu miaka 40,000 iliyopita! sasa historia inajirudia tena, je unataka kuwa sehemu ya historia hii? kwa taarifa zaidi endelea kuangalia EATV ( The nomber one youth channel)