Msanii wa siku nyingi kwenye dambwe hili la muziki wa kizazi kipya kutoka Dodoma ambaye pia ni muasisi wa kundi la chamber squard ambalo linaundwa na Ngwea, Noorah, na Mez B. Unamsoma poa kwa jina Dark Master.
Mchzi amesema kwa sasa hatokuwa anajihusisha na ishu zinazo husu kundi hilo la Chamber squard kama kutakuwa hakuna mkwanja wa kueleweka.
Aliniambia sababu ya kufanya hivi ni kwamba ameona hakuna faida yoyote aliyoipata katika kundi hilo tangu anze muziki huu ambapo sasa ni kama miaka 11 imepita, anasema anaona wengine wanafaidika ambao wapo katika hilo kundi kwa kazi za nje lakini yeye patupu, soo... ameamuwa kufanya kazi zake mwenyewe na kama wana wa kundi hilo watamuhitaji basiiii... inabidi mkwanja utembee kwanza ndio kazi ifanyike.
TRA, ZRA ZAWEKA MIKAKATI YA KUIMARISHA UTENDAJI KAZI WA MIPAKA YA TANZANIA
NA ZAMBIA
-
Na mwandishi wetu Tunduma
KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata na
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zambia (ZRA), Dingani Ban...
8 hours ago
No comments:
Post a Comment
,