.

Thursday, October 29, 2009

KAZI YOYOTE INAHITAJI UMAKINI SANA ILI KUIFANYA KWA UFANISI..

LEO NDIO KINASANUKA A-TOWN KATIKA CRUISE PARTY..

Huyu ni CPWAAAA... alitimba mzigoni kwa ajili ya maandalizi ya bata za Arusha na Moshi.

Leo ni tarehe 30/10/09 ambapo Arusha ndio paleee Masai camp ktakuwa na party kwa ajili ya wajanja wote wa A-TOWN na kwenye stage ni yule yule mkali zaidi yao si mwingine ni mchizi mwenye muonekano wa kiupole sana umesha mfahamu ni nani mchizi anaye fanya vizuri sana katika upande wa Bongo Crank umesha mjuwa niiiii.... CPWAAAAAA... USIKOSE ITAKULA KWAKO...!!!

HUYU NDIO MZEE WA BLOG YA FULL SHANGWE .

Kushoto John Bukuku akiwa na Mpango Mzima (dullah)...Kama uliwahi kutembelea blog ya full shangwe basi huyu ndio kifaru wa huo mzigo kwa habari zaidi tembelea www.fullshangwe.blogspot.com

WHO WILL BE THE ONE AND ONLY M-NET FACE OF AFRICA 2009…


It’s more than a name, more than a moment.

In Africa, for a decade, one search has led the way to find iconic, unforgettable African style.

That search is M-Net’s powerful Face of Africa and this month, the legendary competition returns to television screens once more to tell a story of hope and opportunity, as the journey from Africa’s busy streets to Africa’s glamourous catwalks continues.

From Saturday October 31 at 19.00 CAT (M-Net East), and running 17 weeks, Face of Africa will cross countries, uncover fresh new faces, and chart their rise to the top, from discovery to success, from potential to fame, from possibility to reality. Along the way, audiences will discover how Tanzania’s gorgeous Lillian Alphonce Mduda was discovered at this year’s audition in Dar es Salaam and how far she’s progressed in the competition.

Speaking as M-Net readies itself to screen a new expanded series, Africa Director Biola Alabi was clear on the project’s legacy, its aims and its outcomes.

“Over time, this initiative has shown that it is about so much more than just fashion and beauty. There is a bigger picture there to see, something more than shoes, and cameras and clothing. It’s about young women with so much courage that they will leave their homes to find new experiences, so much determination that they will venture into the unknown to discover themselves, so much passion that they will chase their dreams.”

She goes on to say, “There’s something so magical about this, so special to see, that M-Net wants to share it with audiences across Africa. Because these are Africa’s own and they are taking their chance to shine. We want to laugh with them, cry with them, celebrate with them and now our audiences can do this, every step of the way.”

With a winner prize of USD 50 000 plus a modeling contract with O Model Africa, the new season of Face of Africa began earlier this year with auditions in 14 countries - Angola, Botswana, Ethiopia, Ghana, Kenya, Malawi, Mozambique, Namibia, Nigeria, South Africa, Tanzania, Uganda, Zambia and Zimbabwe. Further entry was open online to entrants from across sub-Saharan Africa who wished to participate gaining entries from as far afield as Sudan and Cameroon. The next step was the casting sessions where a special team of model scouts evaluated entries and selected contestants to continue in the series.

Emotional, dramatic and entertaining, these castings were filmed and audiences will now be able to see behind-the-scenes of the search and live the experience.

At the end of the audition phase, 24 models from16 countries were selected to participate in Model BootCamp, in Mombasa in Kenya. This idyllic tropical paradise with its breathtaking shoreline served as backdrop for another selection round amidst modeling workshops, fashion photo-shoots and television filming.

With some of the selected contestants exiting the competition at this point, the Mombasa BootCamp was action-packed, exciting and a little tense, as contestants learnt, honed their skills and competed to remain in the competition under the watchful eye of BootCamp presenter and former Face of Africa 2005 Kaone Kario.

With stops scheduled in Johannesburg as well as a second Model BootCamp in Dar es Salaam at Swahili Fashion Week, plus the shooting of a music video with Nigerian superstar D’Banj, the Face of Africa adventure will be told every Saturday evening on M-Net East, in the lead-up to the Face of Africa 2009 Finale, to be held in Lagos on Saturday February 6, 2010.

For fans of the series, remember you can also log on to www.mnetafrica.com to watch exclusive footage, find out more about the contestants, access photographs and chat to other fans about this year’s search.

Meanwhile as the search for a new Face of Africa gets underway, last year’s winner Kate Menson is living her dream job. The 24-year-old has been starring in M-Net’s advertising campaign for the new season of Face of Africa and in addition, she recently completed a stay at the Big Brother house. Other credits include appearances at Mozambique Fashion Week, New Delhi Fashion Week, Cape Town Fashion Week and New York Fashion Week, plus she’s appeared on the pages of Elle, Glamour and Cosmopolitan.Now, as Kate continues her rise to the top of the fashion world, a new face is about to be transformed from aspiring model to fully fledged modeling sensation…to find out who, simply follow the search on M-Net.

UMESHAWAHI KULA PWEZA WEWE...???

Huyu jamaa anaitwa Juma yeye anaishi Kigamboni na hiyo ndio biashara yake na kikubwa zaidi jamaa anaijuwa PALNET BONGO kuliko unavyo ijuwa ni nomaaa...

Leo mjini katika mishe mishe za kukimbizana na kitu kinachoitwa pesa, tulifika sehemu tukaweka poz kidogo.. sindio akapita muuza pweza bahati nzuri sasa kumbe yule jamaa muuzaji ni bonge la shabiki wa PLANET BONGO sasa kukawa na shughuli moja tu ya kuwatafuna haoooo pweza ni watamu balaaaaa....
Wenyewe wanasema raha ya pweza chachandu

Josiah Murunga akimsubiri kwa hamu huyo pweza hiyo sasa ni kama round ya pili hivi ya kwanza ilisha gongwa. Lakini wataalam wa mambo wanasema pweza ni dawa ya mambo flani sijui ni kweliiii....???

WAANDAAJI WA HIPHOP NITE / MUSIC & DANCE WAMEKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI LEO.

Sote tuna fahamu kuwa jumamosi hii kutakuwa na usiku wa Hip Hop pale Diamond Jubilee usiku ambao utahusisha wasanii wa Hip Hop kutoka hapa nyumbani na Ufaransa. Leo waandaaji walikutana na waandishi wa habari katiak ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo kwa ajili ya kuwapa mkakati mzima wa usiku huo.

Hawa ndio ma-dancer kutoka Ufaransa ambao watasababisha katika usiku huo wa Hip Hop pale Diamond Jubilee.

Muwakilishi kutoka EATV Josiah Murunga akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari.

Unaweza kumuita Mjombaa ama Mrisho mpoto huyu ni moja kati ya wasanii watakao kuwepo kutowa burudani.

Wednesday, October 28, 2009

UNFAHAMU KUWA JAMAA ANA UNDUGU NA AY.

Huyu ndio Alpha Rwangwira


Si unamjuwa anaitwa AY kutoka Tanzani.

Yule mshindi wa mwaka huu wa Tusker Project Fame Alpha Rwangira ambaye amevuta mpunga wa kutokana na ushindi huo jamaa ni ndugu yake na AY nilipata nafasi ya kuchonga na AY na aliniambia kwamba yule ni mtoto wa mjomba wake ambapo baada ya mama yake AY ndio anafuata baba yake na Alpha Rwangira, duh.. kumbe hawa jamaa dugu moja.
Alpha Rwangira tofauti na kuvuta mkwanja wa nguvu kutokana na ushindi huo wa Tusker Project Fame mchizi pia ana bima ya afya ya kufa mtu, hata akitaka leo apelekwe Marekani kusafishwa meno inawezekana kutokana na hilo dau la bima yake ya afya.

ETIIII.... INAIJUWA HII CHATA...?????????

ETIII... UNAIJUWA HII CHATA...?????

HIZI NI BAADHI YA TUZO ALIZOWAHI KUPATA PROFESSER JAY (KAKA MKUBWA).

KILI MUSIC AWARDS (BEST OF THE YEAR 2005 - 2006)

BBC na RADIO ONE MUZIKI BIGWA TANZANIA (MWIMBAJI BORA WA MWAKA BONGO FLAVA 2004)

HII TUZO ALIIPATA KUTOKANA NA WIMBO WAKE WA NDIO MZEE AMENIAMBIA NAWEZA KUIITA TUZO YA UTAWALA BORA (MAADILI YA VIONGOZI).

GUINNESS BEAT OF THE SEASON AWARD (BEST HIP HOP ARTIST 2001)

KILI TANZANIA MUSIC AWARDS (BEST COMPOSER 2003)

KILI TANZANIA MUSIC AWARDS (BEST HIP HOP ALBUM 2004)

MR & MISS MZUMBE UNIVERSITY TALENT COMPETITION AWARD (BEST PROMOTOR 2002)
Jay aliniambia kwamba tuzo hii aliipata kwa sababu alionyesha ushirikiano na wanafunzi na alifanya show kwa pesa ndogo tofauti na makubaliano soo.. kwa kitendo hicho jamaa waliamuwa kumpa hiyo tuzo.

KILI TANZANIA MUSIC AWARDS (BEST HIP HOP SINGER 2002)

Hii ni tuzo ya IJUMAA AWARDS (BEST HIP HOP ARTIST 2002)

KILI TANZANIA MUSIC AWARDS (BEST SONG WRITER 2008)

KISIMA MUSIC AWARDS (BEST VIDEO-TANZANIA 2006)

HII NI TUZO AMBAYO ALITUNUKIWA NA KIKUNDI CHA MARASTA AMBAO WALIKUBALI KAZI ZAKE WAKATENGENEZA TUZO YA KIASILI KWA AJILI YAKE.

PEARL OF AFRICA MUSIC AWARDS (BEST MALE ARTIST FROM TANZANIA 2007)

HUYU NI KAKA MKUBWA..

Mimi kwa mtazamo wangu nahisi Professer Jay ni mwanamuziki ambaye ana tuzo nyingi zaidi, nilitimba nyumbani kwake na kukuta rundo la tuzo kutoka sehemu mbalai mbali na hii inamaanisha kwamba kaka mkubwa ni mwanamuziki mwenye mafanikio sana katika muziki.

Hizi ni baadhi ya tuzo ambazo kaka mkubwa anazimiliki kutokana na kazi nzuri aliyoifanya.

Professer Jay pia ni moja kati ya wanamuziki wa Hip Hop ambao wamepata nafasi ya kukamua katika show ya Hip Hop Night ndani ya Diamond Jubilee.

FID Q LEO ALITIMBA MZIGONI..


Ngosha the don mchizi kutoka Mwanza Fid q alitia maguu pande hizi leo kwa ajili ya maandalizi ya show itakayo fanyika jumamosi hii tarehe 31/10/09 Diamond Jubilee huu utakuwa ni usiku wa Hip Hop show ambayo itahusisha wasanii kutoka hapa nyumbani na kutoka Ufaransa. Fid q nimoja kati ya wasanii watakao wakilisha katika usiku huo wa Hip Hop paoja na professer jay, wanaume Halisi na Mrisho mpoto.

Fid Q akiwa tari kwa ajili ya kuzungumza na raia wa Africa Mashariki kupitia EATV.

Dominick Nyalifa alikuwepo kwa ajili ya E-News

Hapa tunajiandaa kwa ajili ya kuanza kurecord interview na Fid Q kuhusu show ya Hip Hop Night jumamosi hii.

Tuesday, October 27, 2009

MISHE MISHE ZINAENDELEZWA KATIKA WANAWAKE LIVE SHOW.

Niliwa kukufahamisha kuhusu show inayoongozwa na mwanaharakati wa kike Bongo ambaye pia anafanya kipindi cha Bongo Movie kinachorushwa na EATV, show ambayo inahusu maswala ya wanawake wa kitanzania na pia anapata nafasi ya kuongea na wanawake ambao wapo katika sekta mbali mbali na waliofanikiwa kimaisha kwa ajili ya kuleta chachu ya mafanikio kwa wanawake wengine.
Hapa namzungumzia starring Joyce Kiria Nkongo, nilipata bahati ya kutembelea sehemu ambayo huwa ana record kipindi chake cha Wanawake Live Show na haya ndio yanayojiri huko....

Joyce Kiria Nkongo akifanya mahojiano na Mama Rahma huyu ni mwanamke mjasiliamali ambaye yeye shughuli zake ni kuchoma chapati na mafanikio yote ambayo yeye ameyapata katika maisha yake yametokana na hiyo kazi yake.

Kipindi hiki kinamuhusu kila mwanamke wa kitanzania hapa alikuwa akimuhoji Dinah Ismail (Mhariri gazeti la Tanzania Daima).

Hapa wakijitayarisha tayari kwa kuanza kurecord kipindi cha WANAWAKE LIVE SHOW.

Jamani yule sio keysher kweli mmmhh... embu ngoja nimvute zaidi......

Yeah... ndio mwenyewe kweli duh... kweli hii Wanawake Live Show haiyachi kitu huyu pia ni mwanamke ambaye amepata nafasi ya kuongea mawili matatu kuhusu Wanawake katika kipindi hiko... haya ngoja tuone kikishaanza kuruka hewani....

TEAM NZIMA YA BURUDANI IMESEPA LEO KWENDA ARUSHA NA MOSHI KWA AJILI YA THE CRUISE PARTY..

Hii ndio ndinga ambayo wana wamesepa nayo kwenda Arusha na Moshi kwa ajili ya THE CRUISE PARTY.

Zimebaki siku chache sana kabla ya siku ya burudani kukamili siku ambayo burudani itamuhusu kila mtu aliyoko Arusha ama Moshi... hapa naizungumzia THE CRUISE PARTY tarehe 30/10/09 itakuwa Arusha Masai camp na tarehe 31/10/09 ni ndani ya Moshi Club la Liga. Utamu utaongezwa na CPWAAAAA...

Huyu anaitwa Goga ndio suka ambaye anajukumu la kuhakikisha vijana wanafika salama kwaajili ya makamuzi ya tarehe 30 na 31 Arusha pamoja na Moshi.

Mafuvuuuuuuu....!!!!!! Dj AD mchizi ambaye anasukuma mzigo Eas Africa Radio katika kipindi cha Planet Bongo, Power Jams, The Cruise pamoja na FNL.. Hapa yupo tayari kuingia kwenye ndinga kwa ajili ya kuanza safari ya kwenda Arusha paomoja na Moshi.

Mara unaposifia kwamba duh... hii sauti ya EATV ipo poa basi ujuwe huyu jamaa ndio msababishaji wa hayo maujanja anaitwa Dickson a.k.a Mpalianda anazama kwenye ndinga kwa ajili ya safari ya Arusha na Moshi.

Huyu ndio mfalme wa USWAZI sasa sijui na huko atatafuta wanaoweza kula haraka kwa muda mfupi kama kwenye Uswazi Menyuka sijui mi nahisi tu.... Anaitwa Mussa Hussein yupo tayari kwa safari.

Mchizi anaitwa Tawakal (albab) huyu ni mpiga picha si unamuona hapo yupo kamili na vifaa vyake vya kazi ndio alikuwa anazama kwenye ndinga.

Hawa ni mapacha wasio fanana kushoto ni Dj AD pamoja na Dullah ndani ya ndinga, hawa jamaa huwa una wasoma poa kwenye Planet Bongo ya East Afrika Radio kila jumamosi kuanzia saa nne asubuhi hadi saa sita mchana.

'Jamani huu mfuko ndio kila kitu kama utapotea huu basi safari yenyewe haifai'..... mmh... sasa sijui kuna nini humo.

Si unajuwa safari yoyote haikosi kiongozi hivyo sasa... anaitwa ALEX

Huyu ni Big Man Kim (dj kim) nilipataga story ya huyu jamaa kuwa akisafiri huwa anapenda sana kukaa dirishani leo ndio nimeamini.

Jamani kwa kherini sisi tunaelekea Arusha na Moshi kwaajili ya kuikaribisha familia mpya ya EAST AFRIKA RADIO pamoja na EAST AFRIKA TV (EATV) Arusha na Moshi. Jamani hapa kiatu tu mwanzo mwisho break ya kwanza moshiiiiii haina kula hiyo hawa jamaa watajiju..