Hii ndio ndinga ambayo wana wamesepa nayo kwenda Arusha na Moshi kwa ajili ya THE CRUISE PARTY.
Zimebaki siku chache sana kabla ya siku ya burudani kukamili siku ambayo burudani itamuhusu kila mtu aliyoko Arusha ama Moshi... hapa naizungumzia THE CRUISE PARTY tarehe 30/10/09 itakuwa Arusha Masai camp na tarehe 31/10/09 ni ndani ya Moshi Club la Liga. Utamu utaongezwa na CPWAAAAA...
Huyu anaitwa Goga ndio suka ambaye anajukumu la kuhakikisha vijana wanafika salama kwaajili ya makamuzi ya tarehe 30 na 31 Arusha pamoja na Moshi.
Mafuvuuuuuuu....!!!!!! Dj AD mchizi ambaye anasukuma mzigo Eas Africa Radio katika kipindi cha Planet Bongo, Power Jams, The Cruise pamoja na FNL.. Hapa yupo tayari kuingia kwenye ndinga kwa ajili ya kuanza safari ya kwenda Arusha paomoja na Moshi.
Mara unaposifia kwamba duh... hii sauti ya EATV ipo poa basi ujuwe huyu jamaa ndio msababishaji wa hayo maujanja anaitwa Dickson a.k.a Mpalianda anazama kwenye ndinga kwa ajili ya safari ya Arusha na Moshi.
Huyu ndio mfalme wa USWAZI sasa sijui na huko atatafuta wanaoweza kula haraka kwa muda mfupi kama kwenye Uswazi Menyuka sijui mi nahisi tu.... Anaitwa Mussa Hussein yupo tayari kwa safari.
Mchizi anaitwa Tawakal (albab) huyu ni mpiga picha si unamuona hapo yupo kamili na vifaa vyake vya kazi ndio alikuwa anazama kwenye ndinga.
Hawa ni mapacha wasio fanana kushoto ni Dj AD pamoja na Dullah ndani ya ndinga, hawa jamaa huwa una wasoma poa kwenye Planet Bongo ya East Afrika Radio kila jumamosi kuanzia saa nne asubuhi hadi saa sita mchana.
'Jamani huu mfuko ndio kila kitu kama utapotea huu basi safari yenyewe haifai'..... mmh... sasa sijui kuna nini humo.
Si unajuwa safari yoyote haikosi kiongozi hivyo sasa... anaitwa ALEX
Huyu ni Big Man Kim (dj kim) nilipataga story ya huyu jamaa kuwa akisafiri huwa anapenda sana kukaa dirishani leo ndio nimeamini.
Jamani kwa kherini sisi tunaelekea Arusha na Moshi kwaajili ya kuikaribisha familia mpya ya EAST AFRIKA RADIO pamoja na EAST AFRIKA TV (EATV) Arusha na Moshi. Jamani hapa kiatu tu mwanzo mwisho break ya kwanza moshiiiiii haina kula hiyo hawa jamaa watajiju..
VETA yadhamiria kufikia 50% ya udahili wa wasichana kwenye vyuo vyake
-
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA, Anthony Kasore akizungumza wakati wa
kuhitimisha zoezi la uchaguzi wa wanafunzi walioomba kujiunga na mafunzo ya
ufundi ...
48 minutes ago
Hi kwa washikajiwote wa mpango mzima. im lily
ReplyDelete