Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. William Lukuvi aliitisha kikao cha wasanii wote wa hapa bongo bila kujali ni msanii wa aina gani, awe anaimba anaigiza mchonga vinyago kila aliyekwa msanii alihusika na kikao hicho kilicho fanyika ofisini kwake mitaa ya Ilala Boma.
Nia ya mkuu wa mkoa ni kuwa saidia wasanii kero zao zote zinazohusu kazi zao kuanzia watu wanaoiba kazi za wasanii na kila kitu kinacho wa kwamisha katika kazi zao, Mkuu wa mkoa anasema alikuwa anaangalia EATV kipindi cha Bongo Movie ndipo alipo gunduwa kwamba kuna malalamiko ya wasanii kuhusu mambo yao ndio maana akachukuwa uwamuzi wa kuwakutanisha kwa pamoja ili kusikiliza kero zao. Mwisho kabisa mzee Lukuvi alitoa shukrani kwa EATV kwa kazi nzuri wanayo ifanya iliyo msababisha yeye kuweza kugunduwa hili. Kikao kingine kinafanyika leo 23/10/09 katika ofisi yake saa nane mchana.
No comments:
Post a Comment
,