PLANET BONGO KILA JUMAMOSI SAA NNE ASUBUHI EAST AFRIKA RADIO NA KILA JUMA TANO SAA TATU KAMILI USIKU EATV.
KUWA MAKINI
TULIA NA MMOJA UNAYE MPENDA, ACHA NGONO ZEMBE
POWER JAMS
POWER JAMS,JUMATATU MPAKA IJUMAA KUANZIA SAA 7 MCHANA HADI 10 ALASIRI EAST AFRICA RADIO.
MATING'A
DEEJAY AD a.k.a MAFUVU.
KUTANA NA DEEJAY AD KWENYE POWER JAM KILA J.3 NA ALHAMISI (1:00 - 4:00 pm), THE CRUISE J5 (8:00-9:00 pm), PLANET BONGO JUMAMOSI (10:00 - 12:00 pm) & FNL. NDANI YA EAST AFRICA RADIO & TV, TING'A KALI NAMBA MOJA KWA VIJANA
Hapa namzungumzia Chokoraa, Kalala Jr, Chaz Baba pamoja na Jose Mara.Hawa jamaa wanatoka katika band mbali mbali lakini wamegunduwa kwa umoja wao wanaweza wakafanya kitu kitakacho kuwa burudani kwa raia.
Leo ndio utakuwa utambulisho rasmi wa vijana hawa katika ukumbi wa Java Stereon - Kinondoni mlangoni utasalimisha buku tano tu. TID ni moja kati ya wasanii watakao toa taf kwa mapacha hao.
Mwanamuziki Di Banji katikati wa Nigeria amewasili leo mchana kwenye uwamja wa ndege wa mwalimu J.K.Nyerere kwa ndege ya shirika la ndege la Ethiopia Airline. Mchizi ni moja kati ya wasanii ambao stage itawahusu sana tu juma mosi hii katika viwanja vya Tanganyika Pakers Kawe.
Hii inaitwa Inter-College Special 2009 itakayo sindikizwa na wasanii wengine kutoka Bongo na Kenya, Belle9, Cpwa, Mangwear, Jua kali, Nonini na wengineo wengi kiingilio ni buku tatu jero tu...!!!
Njoo utizame show kali yenye kuunganisha vichwa viwili namzungumzia Fid Q na Mzungu Kichaa, mahali ni pale Russian-Tanzania Cultural Center (Ocean View) kuanzia saa tatu usiku
Katika East afrika tv kuna kipindi kinaitwa 5selekt ni kipindi kinacho wahusu wanafunzi wote wa Aafrika mashariki na kila Alhamis ya mwisho wa mwezi wanafunzi wanasogezewa burudani karibi baada ya kupiga buku kwa muda mrefu sana.
Hilo shangwe ni la Dully ambaye ndio alikuwa na jukumu la kugawa burudani shuleni hapo.
Time ya Shikide ikafika kilichotokea ndio hiki wanafunzi walishindwa kujizuia wakaungana kwenye stage na mr. Shikide.
Hapa sasa mwenye macho haambiwi tazama.
Kweli burudani ndio kila ki2 pamoja na juwa kuwa kali lakini wapi......!!!!!
Unamuona Qeen Doren...!!!
Ndugu hiyo ni fashion show kutoka kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mama Salma Kikwete niskize mm pia....!!!
Kama unavyo juwa mwanzoni kulikuwa na utata kati ya Kallage na Matonya kuhusu maswala ya kazi kama unavyo juwa Kallage ni mtayarishaji wa video hapa bongo na Matonya ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kwa maana hiyo hawa jamaa kazi zao zinategemeana hapo ndipo utata ulipoanza na ilifikia hatuwa walikuwa wanaishi kma paka na panya.
Lakini kwa sasa utata wote kushinei jamaa wameelewana wapo poa sana na katika kuthibitisha hilo kesho tarehe 27 Matonya atafanya video yake ya wimbo wa MARIAM na mchizi Kallage.Lakini kwa mujibu wa Kallage mwenyewe amesema anataka kumalizana na wale wote aliowakwanza mwanzoni akiwamo Lady Jay Dee.
Fununu zinadai kwamba wapinzani wawili Jose Chameleone na Bebe Cool wako studio kurekodi albam ya pamoja. Inasemekana wanataka kutumia njia hii kama njia moja wapo ya kuwawezesha kutikisa tena anga ya muziki Afrika Mashariki. Wimbo wa kwanza pengine kuachiwa ni remix ya wimbo uitwao 'Bogolako' ambao aliuimba Bebe Cool.
Hemed ambaye huimba mahadhi ya RnB, anajipanga kuachia albam yake mchizi pia amenicha kuwa hajashirikisha msanii yoyote.Na sababu ya yeye kufanya hivyo ni kwambaa jamaa anataka kuleta utofauti katika muziki huu wa Bongo Flava. Mzigo utakuwa unaitwa "KING WA MELODY'S sooo....!!!!!! acha tuone yaliyomo yamo....??????
Mchizi alizaliwa 1978 ni moja kati ya ma star wa kimataifa wanao ibuka na kupata mafanikio ya haraka sana katika mchakato mzima wa RAP - MUSIC. Jamaa anatokea SOMALIA lakini alitoroka huko kitambo sana baada ya kukimbia vita vilivyo kuwa vikiendelea huko SOMALIA na kukimbilia TORONTO - CANADA.
K'naan albam yake ya kwanzan ilitoka mwaka 2000 "WHAT NEXT" albam hii ilimpatia mafanikio ingawa sio kivileeee...!!! na kwa sababu ilikuwa ndio mwanzo wake K'naan aliweza kuwa nominated mara tano katika tuzo za huko Toronto zinaitwa Toronto African Music Awards.
Kama unavyo juwa kombe la dunia, jumamosi ya tarehe 21 Nov lilitimba bongo. Na K'naan ni mmoja kati ya watu wanao husika ipasavyo na kombe hilo kila liendapo kwa sababu mchizi yeye ndiye amepata fursa ya kuuandika wimbo Rasmi wa kombe la dunia mwaka huo 2010.
Mimi sio kama nimepewa story no...!! ishu nimeiona live bila chenga, mchezo ulianza hiviiiii....!!! mwanzoni dj choka alikuwa na jazba sana kitendo kilicho fanya kupokea kibano kutoka kwa house boy huyo na maneno kutoka kwa wapambe wa karibu ndio yalikuwa yanazidi kumchefuwa dj choka.
moracka ndio alikuwa mchochezi mkubwa wa kibano hicho cha Dj Choka, mwisho wa siku mm ndio nilio ingilia kati na kumaliza utata huo lakini kwa maelezo ya Dj choka mwenyewe anasema kilicho sababisha kupokea kibano hicho kiulaini ni kutokana na yeye kuto kuwa sio mzoefu wa PLAYSTATION na kingine kikubwa zaidi ni kwamba mchezo waliokuwa wanacheza na house boy huyo ni wa kick box na yeye alikuwa mzembe wa kummiliki mchezaji wake.
kitendo hiko kili pelekea kupokea kibano matata sana kutoka kwa mpinzani (house boy) wake ambaye yeye anaiju vizuri sana game hiyo na alikuwa anamchezesha vizuri mchezaji wake kuliko Dj CHOKA, pole kaka kwa hilo hayo magem tuna cheza sisi tu watoto wa kishua IMEKULA KWAKO......!!!!!
Jamaa tuna mfahamu poa kupitia kundi la Tip Top Connection wengi humuita Bab Tale. Mchizi ameguswa na maneno ambayo yapo kitaa kuhusu washiriki wa shindano hili la BSS kuwa mara baada ya shindano hilo kwisha huwa hakuna chochote kinacho endelea kwa upande wao.
Sooo...!!! mchizi kaona sio ishu sasa anataka kuuthibitishia umma kuwa jamaa wanavipaji na wanaweza kufanya kitu katika huu muziki wa Bongo Flva ndio maana amechukuwa uwamuzi wa kuwagonganisha pamoko kwenye Albam moja.
Tale amesema albam hiyo itahusisha vichwa vitano bora vya BSS ambavyo ni Paschal Cassian wa Mwanza, Beatrice William wa mwanza, Peter Maechi toka mkoa wa Kigoma, Jackson George anayewakilisha mkoa wa Tanga na Kelvin Mbati toka Mkoa wa Dar es Salaam. Mzigo upo chimbo unawekwa sawa ukiwa tayari nitakuhabarisha.
Huyu ni Paschal Cassian ndio mshindi wa BSS kwa mwaka huu.
Itazame vizuri hii tshirt alafu isome na uielewe kisha tazama huo mshale...!!! umegunduwa kitu eeehee...!! basi watu wengi walikuwa hawaja gunduwa hilo na huu mshale uliwahusu sana. huyu dada ni mmoja kati ya waandaaji wa tamasha la BRING IT ON.
Tazama hiyo picha hapo mshale tayari umesha muhusu jamaa lakini alikuwa haja sanuka na hilo mpotezee chek na huyu....
Jamaa naye kajiachia wala hajui kinachoendelea katika flana ya huyo bishosti naye mshale ukamuhusu.
Huyu pia ndani mshale ulimuhusu bila yeye kujuwa, lakini me huwa najiuliza swali moja hiviiii... hizi nguo zenye maandishi kama hii huwa tuna vaa tukijuwa maana yake au wengi wetu huvaa tu kwa ajili ya kijistili....???? lakini me nahisi huyu dada alikuwa ajuwa anacho kifanya na iliwahusu wengi sana hii nguo.
Hapa sasa ni back stage kushoto ni Baby Madaha pamoja na kijana kutoka crew ya Uswazi anaitwa Gelly. Hawa wote walihusika poa katika stage.
Muite PHD, DRY CHAMA au Hemed akiwa na bi shost Angel, Hemedi ni moja kati ya wasanii walio kamua katika tamasha hilo.
Mchizi ambaye anauwezo mkubwa sana katika free style muite God zilla stage pia ilimuhusu.
Jamani hata kama hatuna mvuto wa kupiga picha lakini mara moja moja sio mbya na sisi kuuza si unaona hapo mpango mazima umekamilika naanza mm dullah,Madaha na Gelly.
Haya sasa hapa ndio patam nipo na mrembo Angel, back stage katika tamasha la Bring it on.
Katika tamasha hilo kulikuwa na mashindano kwa wanafunzi mashindano ya kucheza, maigizo, kuimba na mengine mengi na hawa ndio walikuwa ma judge si unamuona luchi (mwenye mawani)
Huyu ni mbunge wa Ilala Mh. Mussa Azan 'Zungu' ndio alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo.
Wanafunzi walipata muda wa kupiga picha na wasanii walio kamua siku hiyo, huyo ni TID akiwa na wanafunzi wa shule mbali mbali.
Hawa ni wanafunzi wa shule ya Makongo wakiwa wanajiandaa kwa ajili ya kuingia ndani na kuungana na wenzao katika tamasha la Bring it on Diamond Jubilee.
Kwa sababu ishu ilikuwa inahusu wanafunzi basiiiii...!!!! mtu mzima Allan Lucky, Skonga ili mlazimisha yeye kuwepo hapo coz.. Skonga ni kipindi kinacho husu wanafunzi na walihusika nacho poa sana kipindi hiko.
Mpango mzima wa Skonga ulikuwa ukiendelea kwa style hii.
BRING IT ON ni tamasha linaliwakutanisha wanafunzi kwa pamoja katika upande wa burudani litafanyika ijumaa hii pale Diamond Jubilee na kushirikisha wasanii tofauti wa Bongo flava, yupo Hemedi, God Zila, Dully Sykes, Baby Madaha na wengine wengi.
Unaweza kumuita PHD au dry chama na sijajuwa sababu ya mchizi kujiita hivyo lakini itabidi nimuulize kuhusu hili ni moja kati ya wasanii watakao kamuwa ijumaa hii Diamon Jubilee.
Huyu mchizi anaitwa Said ni moja kati ya waandaajia wa hilo dude latakalo fanyika ijumaa hii, alikuwa katika interview na Sam katika Power Jams leo mchana.
Mchizi kutoka Dodoma namzungumzia Mangwear tayari amesha dondosha mzigo kitaa soo... hii ndio time ya kuonyesha uzalendo kwa kuacha kununuwa copy fake na kuwawezesha wasanii wetu kufika hatuwa ya kuridhisha zaidi sasa cha kufanya ni kutafuta copy yako ili uwe moja kati ya watu wanaotaka kuinuwa muziki wetu wa kizazi kipya.
Naomi Cambell akihusika poa katika jukwaa, wakati wa onesho maalum lililoandaliwa na Taasisi ya kimataifa yab The White Ribbon Alliance for safe motherhood(WRA) nchini lillilofanyika jana usiku katika hoteli ya movenpick jijini Dar es salaam , kampeni hii inalenga kuhamasisha afya ya mama na mtoto mara baada ya kujifungua.
Huyu ni mchizi kutoka EATV anaitwa Deogratius Kithama akifanya mahojiano na Naomi Cambell jana usiku katika onesho la mavazi la The White Ribbon Alliance for safe Motherhood
Mke wa Rais mama Salma Kikwete akiongea na Mwanamitindo wa kimataifa Naomi Cambell wakati wa onyesho la mavazi la The White Ribbon Alliance for safe Motherhood lililofanyika kwenye Hoteli ya Movenpick
Baba wa Michael Jackson, Joe Jackson amepigwa chini katika kurithi mali za mwanaye lakini anaweza akapata allowance. Jaji wa mahakama amesema jina la mshua huyo halijawekwa katika mirathi lakini atakuwa anapewa kidogo fedha za matumizi. Joe ndio alikuwa mstari wa mbele katika kutoa mafunzo na kuanzisha kundi landugu watano la The Jackson 5, kundi ambalo ndio lilikuwa mwanzo wa Michael Jackson kupata umaarufu duniani kote.
Bondia Mike Tyson amesekwa rumande kwa kosa la kumpiga ngumi mwandishi wa habari. Tyson alikuwa akipigwa picha na paparazzi jijini Los Angeles akiwa na familia yake kitendo ambacho kilimkasirisha na kuamua kurusha ngumi. Paparazzi huyo ilibidi akimbizwe hospitali kwa sababu alivunjika pua... huo ndio mkwaju wa bwana mkubwa Tyson na kama angekuwa bongo duh...!!! hospitali zingejaa kwa sababu najuwa bongo kwa picha tuuu hatu jambo.
NI WEWE KAMPENI, MAENEO YA ITUNUNDU PAWAGA JANA
-
Ni Wewe ni kampeni iliyozinduliwa na redio Ebony FM iliyoko Nyanda za juu
kusini, ikiwalenga zaidi wananchi wa vijijini ambao miundo mbinu ya umeme ...
HARD PRICE COMING SOON
-
* Samahanini sana wadau wangu... Naombeni sana mnisamehe kwa kupotea kwa
kipindi kirefu, na yote haya yanatokana na majukumu ya hapa na pale. Ila
nisinge...