.

Sunday, November 8, 2009

CLUB MAISHA YATEKETEA KWA MOTO MCHANA HUU...

Hapa ndio ile sehemu ya dancing floor na hivi ndivyo inavyoonekana kwa sasa.

duh...!!!! hapa ndio sehemu ya kuingilia Club Maisha ikiwa imeteketea vibaya kwa moto huo.

Mmiliki wa Club Maisha, Mama Hellen sweya akiliwazwa na baadhi ya watu waliofika eneo latukio.

Sehemu ya nje ya Club Maisha hapa gari la zima moto lilikuwa limeshafika.

Kwa wanaoijuwa Club Maisha watakuwa wanapafahamu hapa hii nisehemu ya VIP ambapo ndipo watu huvuta sigara kwa ndani na sasa kunaonekana hivi baada ya moto huo.

Club maarufu ya maisha leo mchana imeteketea kwa moto na inasemekana chanzo cha moto huo ni shot ya umeme inasemekana kwamba kulikuwa na matengenezo ya (AC) sasa katika zoezi hilo kuna nyaya ziligusana ndio ilisababisha mlipuko kutoka katika hiyo (AC) na kusababisha moto huo na kuteketeza kila ktu katika Club hiyo maarufu kwa burudani hapa mjini.

No comments:

Post a Comment

,