.

Tuesday, November 10, 2009

KWANZA MKWANJA ALAFU KUJUANA BAADAYE...!!!!

Msanii wa siku nyingi kwenye dambwe hili la muziki wa kizazi kipya kutoka Dodoma ambaye pia ni muasisi wa kundi la chamber squard ambalo linaundwa na Ngwea, Noorah, na Mez B. Unamsoma poa kwa jina Dark Master.
Mchzi amesema kwa sasa hatokuwa anajihusisha na ishu zinazo husu kundi hilo la Chamber squard kama kutakuwa hakuna mkwanja wa kueleweka.
Aliniambia sababu ya kufanya hivi ni kwamba ameona hakuna faida yoyote aliyoipata katika kundi hilo tangu anze muziki huu ambapo sasa ni kama miaka 11 imepita, anasema anaona wengine wanafaidika ambao wapo katika hilo kundi kwa kazi za nje lakini yeye patupu, soo... ameamuwa kufanya kazi zake mwenyewe na kama wana wa kundi hilo watamuhitaji basiiii... inabidi mkwanja utembee kwanza ndio kazi ifanyike.

No comments:

Post a Comment

,