.

Wednesday, November 4, 2009

VITA YA WEZI WA KAZI ZA WASANII INAENDELEA..

Huyu ndiyo Rich One wa TMK Wanaume Halisi

Leo nilikutanan na Rich One kutoka TMK Wanaume Halisi na aliniambia kuwa wiki iliyopita walipewa taarifa na msamalia mwema kuhusu mwizi wa kazi zao, wizi ambao unafanywa na raia mmoja mwenye asilia kihindi.
Aliniambia msamalia huyo mwema aliwaambia kuwa huyo muhindi anamtambo ndani wa kutengeneza kopy za kazi zao pamoja na wasanii wengine, baada ya kupokea taarifa hizo Rich One pamoja na wasanii wengine wa TMK Wanaume Halisi walienda COSOTA na wakapewa kibali cha kumkamata mtu huyo na sasa kesi bado inaendelea.


HIKI NDICHO KIBALI WALICHOPEWA NA COSOTA SAMAHANI WADAU PICHA HII HAINA MUONEKANO MZURI NI KWA SABABU ZA KIUFUNDI "KAMA UKIHITAJI KUISOMA KWA UZURI ZAIDI BONYEZA HAPO KATIKA HIYO PICHA YA KIBALI"

USHAURI KUTOKA "MPANGO MZIMA" KAMA KUNA MTU YOYOTE UNAYE JUWA KUWA ANAHUSIKA NA HIZI ISHU TAFADHALI TOA TAARIFA KWA WAHUSIKA ILI KUPUNGUZA TATIZO HILI LA WIZI WA KAZI ZA WASANII WETU KAMA TUKISHIRIKIANA KWA PAMOJA LINAWEZEKANA.

No comments:

Post a Comment

,