.

Sunday, November 1, 2009

AJALI KAZINI..

Nilikutana na Producer kutoka pande za Kariakoo katika studio ya Fish Crub hapa na mazungumzia Lamar, tulikutana viwanja flani hivi na alinihabarisha kuhusu ishu ambayo imetokea studio kwake aliniambia Hard disk yake imezinguwa na imefuta kila kitu kilichomo pia aliniambia kuwa humo ndio kulikuwa na Albam za wasanii pamoja na matangazo ya makampuni tofauti. Alisema Albam ya Young d, Fatma pamoja na Geez Mabovu zote zimefutika kwa hiyo ni kama anaanza tena hivii duh.... Lamar mpango mzima inakupa pole sana ndugu yangu hiyo ndio mitihani ya maisha

1 comment:

  1. Pole sana Lamar.
    Pengine la kutambua ni kuwa haya madubwana (Kompyuta) huwa yanatibuka saana na kufuta karibu kila kilichopo. Na kwa kuwa Lamar ni mchapakazi mkubwa na anajua kuwa ana mali za watu ambao wanamtegemea kuwapa wakati fulani, ni vema akawa na BACK-UP ya kusaidia iwapo tatizo kama hili linatokea.
    Akiwa na External Hard Drive ya telebytes kadhaa akawa ana-store kila anachotengeneza na kisha akimaliza anaweza kuhamishia kwenye CD ku-free up nafasi kwenye disk yake itamsaidia.
    Hakuna lisilo na funzo, na naamini hili limekuwa funzo kwake na yawezekana limetokea wakati huu ambao hajawa na wateja wengi wanaotegemea kazi zao karibuni
    POLE SANA Lamar na kuna njia ya kutatua hilo.
    Pengine kuzuia lisitokee kwa mara ya tena ndio mafanikio.
    Nelson Mandela alisema "The greatest Glory in living lies not in never falling, but in rising everytime we fall"

    Blessings

    ReplyDelete

,