.

Monday, November 23, 2009

BABU TALE AKUTANISHA VICHWA VITANO BORA VYA BONGO STAR SEARCH 2009.

Jamaa tuna mfahamu poa kupitia kundi la Tip Top Connection wengi humuita Bab Tale. Mchizi ameguswa na maneno ambayo yapo kitaa kuhusu washiriki wa shindano hili la BSS kuwa mara baada ya shindano hilo kwisha huwa hakuna chochote kinacho endelea kwa upande wao.

Sooo...!!! mchizi kaona sio ishu sasa anataka kuuthibitishia umma kuwa jamaa wanavipaji na wanaweza kufanya kitu katika huu muziki wa Bongo Flva ndio maana amechukuwa uwamuzi wa kuwagonganisha pamoko kwenye Albam moja.


Tale amesema albam hiyo itahusisha vichwa vitano bora vya BSS ambavyo ni Paschal Cassian wa Mwanza, Beatrice William wa mwanza, Peter Maechi toka mkoa wa Kigoma, Jackson George anayewakilisha mkoa wa Tanga na Kelvin Mbati toka Mkoa wa Dar es Salaam. Mzigo upo chimbo unawekwa sawa ukiwa tayari nitakuhabarisha.


Huyu ni Paschal Cassian ndio mshindi wa BSS kwa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

,